header

nmb

nmb

Thursday, January 26, 2012

Wananchi wauwa jambazi Arusha



Na Gladness Mushi wa Fullshangwe - ARUSHA


Mtu mmoja anaesadikiwa kuwa ni jambazi ameuwawa na wananchi wenye hasira kali baada ya kutuhumiwa kuvunja Grocery na kuiba.





Akithibitisha kutokea kwa tukio hilo kamanda wa polisi mkoani hapa Thobias Andengenye alisema kuwa tukio hilo lilitokea January 25 mwaka huu majira ya saa 9:00 usiku katika kijiji cha Kiranyi kilichopo katika halimashauri ya jiji la Arusha mkoani hapa.





Alisema kuwa mtu huyo aliyejulikana kwa jina la John Raphael Mrema anaekadiriwa kuwa na miaka 25-30 aliuwawa na wanchi wenye hasira kali baada ya kutuhumiwa kukvamia grocery na kuiba.




Alisema kuwa kwa mujibu wa taarifa ambazo jeshi la polisi zimezipata zinasema kuwa siku ya tukio marehmeu akiwa na wenzake ambao hidadi yao haijajulikana ambao walishirikiana kuvunja grocery ya mtu aliejulikana kwa jina la Eva Katapa (26) mfanyabiashara na kuiba vivyaji mbalimbali pamoja na fedha taslimu kiasi cha shilingi laki 600,000.




“Sasa baada ya majambazi hawa kuiba katika grocery hiyo ya kwanza waliamia katika grocery ingine ambayo ipo jirani ambapo hapo pia walivunja grill lakini kwa bahati nzuri pale hawakuweza kuchukuwa kitu chochote baada ya majirani kuamka na kufanikiwa kumkamata ndugu John Raphael ambapo walianza kumshambulia kwa kupiga hadi kuuua huku wenzake wakiwa wamekimbia”alsiema Andengenye.




Kamanda wa polisi alibainisha kuwa mpaka sasa hakuna mtu aliyekamatwa kuhusiana na tukio hilo na jeshi la polisi mkoani Arusha linaendlea na upelelezi kuwasaka waliokimbia .




“Mwili wa marehemu umehifathiwa katika hospitali ya mkoa ya Mount Meru hadi hapo ndugu wa marehemu watakapo kuja kuuchukua na pia upelelezi unaendelea “alisema Andengenye

No comments:

Post a Comment