header

nmb

nmb

Wednesday, January 25, 2012

NSSF YA KUSANYA ZAIDI YA BILIONI 16

Na Gladness Mushi wa Fullshangwe -Arusha


MFUKO wa hifadhi ya jamii( NSSF)mkoani Arusha umefanikiwa kukusanya shilingi bilioni 16.745 kwa kipindi cha Jully hadi desemba 2011 ambapo fedha hizo ni sawa na asilimia 92 ya lengo walilokusudia Hayo yalisemwa na meneja kiongozi wa mfuko huo mkoani hapa Bw Jackton Ochieng' alipokuwa akiongea na gazeti hili kuhusiana na hali ya mfuko huo .ilivyo kwa sasa. Aidha alisema kuwa mfuko huo umeweza kuandikisha wanachama 3582 ambapo ni sawa na asilimia 49.8 ambapo hilo ndilo lengo hailsi Vile vile aliongeza kuwa kwa kipindi hicho pia wameweza kuandikisha waajiri 72 ambapo ni sawa na asilimia 79 ya lengo Hata hivyo bw Ochieng' alieleza kuwa mfuko huo umeweza kulipa mafao kwa wanachama wake 2416 ambapo kifedha wamelipwa shilingi bilioni 4033.65. Alieleza changamoto zinazoukabili mfuko huo kuwa ni pamoja na watu kutojua dhana ya elimu ya mfuko wa jamii na hivyo kuwafanya kuwa waoga kujiunga na mfuko huo ambapo alisema kuwa hadi sasa wamejitahidi kutoa elimu hiyo kwa waajiri 53 . Aliitaja changamoto nyingine kuwa ni pamoja na baadhi ya wafanyakazi kurubuniwa na waajiri hali ambayo inaleta matatizo katika mfuko huo. Aliwataka wanachama na wasio wanachama kutokubali kurubuniwa na waajiri kwa kuwa ni haki ya mfuko kuhudumia wanachama wake kuanzia sasa na hata uzeeni .


No comments:

Post a Comment