header

nmb

nmb

Tuesday, January 17, 2012

Mwanafunzi ajiua Arusha kwa kosa la kusingiziwa kuiba dola 1500Na Gladness Mushi wa Fullshangwe- Arusha Mwanafunzi aliyefahamika kwa jina la John Justine(17) mkazi wa makao mapya amefariki dunia jana katika hospitali ya mount meru wakati akipatiwa matibabu baada ya kujeruhiwa kwa risasi. Akizungumza na wandishi wa habari kamishina msaidizi mwandamizi wa jeshi la polisi mkoa arusha Thobias Andeng'enye amesema kuwa tukio hilo lilitokea majira ya saa moja na nusu jioni ambapo siku hiyo mama wa marehemu aitwaye Betty John alikuwa akitoka kwenye sherehe mara baada ya kufika nyumbani alikuta geti limefungwa ndipo alipowaomba majirani kumsaidia kufungua. Andeng'enye amesema kuwa mama huyo amesema kuwa mara baada ya kuingia ndani akiwa na mtoto wa jirani alimkuta mtoto wake akiwa chini amelala chini huku akihema kwa tabu huku damu zikimtoka kifuani ndipo alipotoka nje na kuomba msaada kwa majirani. Aidha kamanda alisema kuwa mma huyo pamoja na majirani walisaidina kumkimbiza hospitali ya Dkt.Mohamed iliyopo eneo la Tank la maji Ilboru kwa matibabu ambapo ilishindikana na kumpeleka hospitali ya mkoa ya mount meru ambapo ailipatiwa msaada lakini kwa bahati mbaya alifariki dunia. Hata hivyo andeng'enye amesema kuwa baada ya polisi kituo kikuu wilaya kupata taarifa walikwenda eneo la tukio kufanya ukakuzi ambapo walikuta bunduki aina ya shortgun Pump Action pamija na ujumbe unaosema"ANASIKITIKA KULAUMIWA NA WAZAZI WAKE PIA ANAWAPENDA SANA" Vilevile walikuta michirizi ya damu kutoka chumbani hadi alipoangukia. Kamanda ameongeza kuwa inasemekana kuwa marehemu alituhumiwa na baba yake mzazi Jastine Kaizer kuwa aliiba fedha kiasi cha dola za marekani 1500 hivyo polisi bado wanaendelea na uchunguzi wa kumhoji baba mzazi wa marehemu . Mwili wa marehemu umehifadhiwa katika chumba cha maiti cha mount meru ukisubiri uchunguzi zaidi wa daktari.

No comments:

Post a Comment