Mwenyekiti wa Taifa wa Jumuia ya Wazazi ya CCM, Balozi Athumani Mhina enzi za uhai wake. Katibu Mkuu wa Jumuia hiyo, Khamis Dadi alisema Balozi Mhina alifariki usiku wa kuamkia jana aliokuwa akipelekwa katika Hospitali ya Jeshi Lugalo kutibiwa shinikizo la damu. Dadi alisema Mhina alikuwa akipelekwa hospitali baada ya hali yake kubadilika ghafla kutokana na maradhi ya shinikizo la damu.Alisema mwili wa marehemu, ambaye pia alikuwa Mjumbe wa Kamati Kuu na Halmashauri Kuu ya CCM, umehifadhiwa katika Hospitali ya Jeshi ya Lugalo na kwamba mazishi yake yanatarajiwa kufanyika leo. Dadi alisema marehemu atazikwa kijijini kwao Mnyuzi wilaya ya Korogwe mkoani Tanga na kwamba mwili wake ulisafirishwa jana kwenda kijijini huko. Alisema kabla ya kusafirishwa, wakazi wa Dar es Salaam walipata fursa ya kutoa heshima za mwisho nyumbani kwake Madale, Tegeta wilayani Kinondoni. Kwa hisani ya fullshagwe blog
No comments:
Post a Comment