Wanaharakati nchini Misri wametoa wito kwa wananchi kuungana katika maandamano makubwa katikati mwa mji mkuu, Cairo hii leo.
Lengo ni kuushinikiza utawala wa kijeshi kuachia madaraka .
Awali, Baraza la mawaziri la kiraia nchini Misri liliwasilisha ombi la kujiuzulu kwa baraza la utawala wa kijeshi, huku maelfu ya waandamanaji wanaopinga utawala huo wakikita kambi kwenye medani ya Tahrir mjini Cairo .
Shirika la kimataifa la kutetea haki za binadamu, Amnesty International, limewashutumu vikali watawala wa kijeshi wa Misri, likisema wamepoteza matumaini ya waandamanaji wanaopigania demokrasia na kushindwa kabisa kutimiza ahadi zao za kuboresha haki za binaadamu.
Shirika hilo linasema baraza kuu la kijeshi la Misri limeendeleza utawala wa uonevu ambao Misri ilishuhudia chini ya Rais Hosni Mubarak, ambaye alipinduliwa mwezi Februari mwaka huu.
Ripoti hiyo imetolewa kufuatia siku kadhaa za ghasia za makabiliano baina ya vikosi vya usalama na waandamanaji mjini cairo ambapo watu zaidi ya 20 waliuawa.
No comments:
Post a Comment