header

nmb

nmb

Wednesday, November 23, 2011

Baada ya kustaafu alitegemea apumzike ajitafunie bata lakini kizaizai chaanza mahakamani!!



ALIYEKUWA Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya Ndege Tanzania (ATCL) David Mattaka - pichani na vigogo wenzake wawili wa zamani wa shirika hilo, wamefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar es Salaam jana wakidaiwa kununua magari chakavu 26 kinyume cha sheria ya ununuzi. Washitakiwa wengine ni aliyekuwa Kaimu Mhasibu Mkuu, Eliasaph Ikomba na aliyekuwa Mkurugenzi wa Mahesabu, William Haji. Washitakiwa hao jana walisomewa mashitaka na waendesha mashitaka kutoka Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU), Ben Lincon na Osward Tibabyekomya, na baadaye kuachiwa kwa dhamana walipotimiza masharti.
Mattaka jamani mattaka!!.Hatuna cha Kuongeza kwani jambno liko mahakamani

No comments:

Post a Comment