header

nmb

nmb

Monday, October 31, 2011

Mlinzi aliyepigwa shoka la kichwa haliyake bado tete Moi muhimbili!!

Hali ya Mlinzi aliyepigwa shoka huko tabata mwishoni mwa wiki na shoka hiyo kubaki kichwani anaendelkea kupumua kwa kudura za mwenyezi mungu. katika hali ya kushangaza na kyupelekea jina la mungu kubaki kuwa mungu soma kisa hiki kwa undani.Wadau picha hizi zinatisha lakini mtuwie radhi kwani ndiyo hali halisi iliyotokea usiku wa kuamkia leo huko Tabata na hakuna mtu anayeweza kuvumilia maovu haya yanaofanywa na watu wasiokuwa na utu. Leo saa 12 asubuhi hospitali ya taifa Muhimbili imempokea mgonjwa anayeitwa Mussa Shabani(42) akiwa na shoka iliyonasa kichwani

(kama picha inavyooneka hapo chini).

Bwana Mussa ni mlinzi katika nyumba ya Joseph Mwakyusa huko Tabata. Majambazi yalipofika nyumbani kwa bawana


Mwakyusa yalimjeruhi

kwa shoka bwana mussa na, wakati majambazi yaliyovamia nyumba ya Mwakyusa yakiendelea kufungua spea za gari aina ya Toyota verosa. kwa bahati nzuri bwana Mwakyusa alishtuka

na ndipo

majambazi hayo yalipokimbia na kutoweka yakimuacha mussa katika hali mbaya na shoka ikiwa imenasa kichwani.


Madaktari wa taasisi ya tiba ya mifupa MOI walifanya kazi ya ziada kuitoa shoka hiyo na sasa Mussa yupo chumba cha wagonjwa

mahututi. bwana.

Jumaa Almasi afisa uhusiano mkuu wa MOI amethibitisha tukio hilo na kusema ''Ni kweli bwana Mussa amepokelewa hapa MOI akiwa na shoka iliyonasia


kichwani mwake lakini madaktari wamemfanyia upasuaji na kuitoa na sasa hivi yupo chumba cha Mahututi

No comments:

Post a Comment