header

nmb

nmb

Thursday, March 10, 2011

WANAFUNZI WA CHUO CHA UUGUZI MTWARA WATOA KILIO CHAO KWA WAZIRI

Dkt. Hadji Mponda akiongea na wanafunzi wa chuo cha uuguzi na ukunga cha Mkomaindo,wanafunzi hao walisema kero yao kubwa inayowakabiri chuoni hapo ni ukosefu wa mabweni,kompyuta.maji pamoja na walimu,aidha Waziri wa Afya na Ustawi wa jamii aliwaahidi kushughulikia matatizo hayo.

Wanafunzi wa Chuo hicho wakishangilia baada ya Waziri wa Afya na Ustawi wa jamii kuingia chuoni hapo kujionea mazingira ya chuo hicho.

Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii Dkt. Hadji Mponda akisikiliza malalamiko ya wagonjwa waliofika kupata matibabu katika hospitali ya Wilaya ya Mkomaindo iliyopo Masasi,nje ya chumba cha x-ray,wagonjwa hao licha ya kutoa kilio chao juu ya matibabu pia walishauri Serikali iongeze idadi ya watumishi katika hospitali hiyo.

Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii Dkt. Hadji Mponda akiagana na wanachuo hao mara baada ya kutembelea chuo hicho chenye zaidi wa wanafunzi 100 ambapo aliwatoa wasiwasi wa kupata ajira kwani ajira yao inatolewa moja kwa moja kwa wahitimu wa kada za afya nchini.(Picha zote na caherine Sungura-MOHSW).

No comments:

Post a Comment