header

nmb

nmb

Wednesday, March 9, 2011

Mfuko wa Aranyande, waanzishwa kusaidia watoto yatima!

Matukio OleAfrika Aranyande Chuma akiongea na waandishi wa habari ktk uzinduzi wa Mfuko huo leo ktk kijiji cha Makumbusho jijini DSM.

Mfuko wa Aranyande ambao nauzindua leo hii si dhana iliyoanza jana au leo bali kwa miaka kadhaa kupitia vituo mbalimbali na kusomesha watoto kadhaa katika ngazi tofauti tofauti lakini imefika kipindi ambacho nimeona ni wakati muafaka kwa kila mtanzania kuamua na kutambua umuhimu wa kujitolea katika kusaidia wale wasio na uwezo ili kusukuma gurudumu la maendeleo ya Taifa letu. Si wakati wa kulalama, kulaumu ama kukata tamaa peke yake bali kujitoa, kujitambua na kubwa zaidi kuchukua hatua. Kama kuna mwenye majukumu lakini yeye akachagua kudharau, kubeza, kuwa na kiburi na wingi wa zenye kukera kauli, haina maana na wala haitosaidia kama taifa kwetu sote kuamua kukaa kimya ama kulalama na kulaumu peke yake bali wengi walio weledi husema muungwana ni kitendo.

Popote tulipo katika dunia hii jadidu tutambue kuwa sisi ni watanzania, kujikana, kujisahaulisha au kuamua tu kusahau kwa kusudi zenye tambo na kebehi haisaidii wala kuokoa taifa leu bali ni sawa na kuwa abiria kwenye chombo na kukaa kimya angali hatari au uongezeko wa matatizo katika jamii yetu hasa kwa wale wasiojiweza ikiongezeka.

Mfuko wa Aranyade ni mfuko utakaotoa angalau ufadhili kwa watoto wawili kila mwaka kwa mwaka mzima katika suala zima la malipo ya masomo ili changamoto tuzipatazo kwa kukosa wazazi, walezi, uwezo, makundi tengwa katika jamii nakadhalika zisiwe chachu ya kutukosesha kile kilicho cha msingi kabisa katika maisha yetu yanatukabili yaani elimu.

Mfuko huu utaratibiwa kwa ushirikiano mkubwa na The East Africa Speakers Bureau amabo hawa ni mabingwa katika nyanja ya uratibu, semina elekezi na zenye wingi wa mafunzo ya nyanja mbalimbali vilevile makongamano na shughuli zifanywazo kwa umakini wa hali ya juu. Shukrani za kipekee ziende kwao na timu yao yote kwa kukubali kusimamia na kuratibu zoezi hili hasa katika kipindi hiki japo wana majukumu makubwa na mengi lakini mchango wao katika yale yahusuyo ueledi na uendelevu na mtu mmoja mmoja na taifa kwa ujumla halina kificho bali wingi wa utekelezaji.

Mfuko wa Aranyande pia na shughuli nzima ya leo haungeweza kuwa mafanikio kama si ushirikiano wa kutosha kutoka kwa msanii nguli, mwenye wingi wa sanaa liyojaa mafundisho, burudani inakishwayo na midundo ya kiasili ya nchi yetu tukufu ya Tanzania, sio mwingine napenda kumwita Shangazi aliyejaa wingi wa hekima na mashairi yale vilivyojipanga vina, Irene Sanga.

No comments:

Post a Comment