Tarehe 17/10/2010 Tagawa Lions Club iliyopo katika mji wa Tagawa, mkoa wa Fukuoka, nchini Japan ilifanya sherehe ya kuadhimisha miaka 50 tangu kuanzishwa kwake. Sherehe hizo zilihudhuriwa na Balozi wa Tanzania nchini Japan Mhe. Salome T. Sijaona. Klabu hiyo itaendelea kutekeleza shughuli mbalimbali kama sehemu za maadhimisho hayo. Moja ya shughuli hizo ni kuwaalika wasanii wa michoro ya Tingatinga kutoka Tanzania kuja kufanya maonyesho ya kuchora katika mji huo na kuuza michoro watakayoiandaa. Huo ni mkakati mpya wa kuanzisha uhusiano wa kiutamaduni kati ya mji huo na Tanzania. Aidha, ni njia nzuri ya kuitangaza sanaa ya Tingatinga nchini Japan.
Katika picha ni Balozi Sijaona akiwa na viongozi wa Tagawa Lions Club pamoja na Meya wa mji wa Tagawa.
No comments:
Post a Comment