header

nmb

nmb

Friday, October 22, 2010

MWISHO MWAMPAMBA AFAFANUA KUHUSU MKEWE MTARAJIWA

Mwisho Mwampamba akizungumza na waandishi wa habari leo kwenye Hoteli ya Holliday Inn ya jijini Dar es salaam mara baada ya kurejea kutoka Afrika Kusini alikokuwa akishiriki katika shindano la BigBrother Africa Allstars lililomalizika wiki iliyopita nchini Afrika Kusini ambapo Uti mshiriki kutoka nchini Nigeria alikuwa ndiye mshindi na kujinyakulia kitita cha Dolla za Kimarekani laki mbili. Mwisho amesema japokuwa hakushinda lakini anajisikia kwamba hajakosa chochote kwakuwa ammepata uzoefu wa mambo mbalimbali na kujifunza mambo mengi akiwa kwenye jumba la BigBrother hivyo hilo pia ni jambom la kumshukuru mungu kwa yote. Ameongeza kwamba anashukuru kwa kupata nafasi nyingine hii na ataitumia vyema katika mambo mbalimbali na changamoto zilizoko mbele yake katika kutekeleza majukumu yake. Mwisho Amwulizwa swali mwandishi wa habari wa Champiaon Saleh Ally juu ya maamdalizi ya harusi yao na Merry mara baada ya yeye kumvisha pete ya uchuma mrembo huyo ndani ya jumba la BigBrother Mwisho amesema. "Ukitaka kujua Utamu wa Ngoma Shurti Uingia Ucheze, Siwezi kuzungumzia lolote kuhusu Mwenzangu kwani jambo hili linatuhusu wote wawili, lakini kama angekuwepo tungeweza kujibu chochote juu ya hilo hivyo siwezi kusema chochote juu ya mipango yetu". Katika Picha kushoto ni Meneja Masoko wa Mulitchice Furaha Samalu.
Waandishi wa habari kutoka vyombo mbalimbali wakiwa katika mkutano wakati mwisho alipoongea na waandishi wa habari leo kwenye hoteli ya Holliday Inn jijini Dar es salaam.Kwa hisani ya Full shangwe

No comments:

Post a Comment