header

nmb

nmb

Friday, October 29, 2010

DKT. KIKWETE .DKT. SLAA ,WASIFU WAO KWA UFYPI!!

Dkt Jakaya alizaliwa 7 Oktoba, 1950 katika kijiji cha Msoga, kata ya Lugoba, tarafa ya Msoga, Jimbo la Chalinze, Wilaya ya Bagamoyo, mkoa wa Pwani. Lugha ya mama ilikuwa Kikwere. Alizaliwa katika familia ya wanasiasa. Babu yake Mzee Mrisho Kikwete alikuwa chifu wa Wakwere. Baba yake alikuwa Mkuu wa Wilaya Pangani, Same na Tanga. Jakaya Kikwete amesimulia hadithi ya kifamilia ya kuwa wakati mama yake alipokuwa mja mzito naye, Babu alitamka kuwa ikiwa mtoto atakuwa wa kiume atampatia urithi wa cheo chake.

Dk Slaa alizaliwa Oktoba 29, mwaka 1948 wilayani Karatu. Alipata elimu ya msingi katika shule za Karatu na Kwermusi (Mbulu) kati ya mwaka 1958 na 1965.

Alisoma elimu ya sekondari katika Shule za Dung’unyi Seminari na Itega Seminari kati ya mwaka 1966 na 1971.hadi sasa ni Katibu Mkuu wa Chadema pia aliwahi kuwa mbunge kwa miaka 15

No comments:

Post a Comment