Ama kweli dunia uwanja wa mapambano! Skendo motomoto iliyoenezwa mtandaoni ikidai kuwa Super Model, Jokate Mwegelo na nyota wa mpira wa kikapu anayekipiga katika ligi ya NBA Memphis, Marekani, Hasheem Thabeet Manka kuwa wanaishi wote, ni ya kupikwa, Ijumaa linakupa kitu kamili.
Kwa mujibu wa habari kutoka mtandao mmoja (jina tunaminya), Jokate yuko nchini Marekani ambako anaishi na staa huyo wa kikapu jambo ambalo Hasheem amekuja juu na kulikanusha kwa nguvu zote.
Katika habari hiyo iliyopewa kichwa: “MISS AHAMIA MAREKANI KUISHI NA HASHEEM THABEET”, ilisomeka hivi:
“Golden Boy, Hasheem Thabeet yuko ‘deep in love’ na binti wa kibongo. Mapenzi hayo yalianza mienzi michache iliyopita Hasheem alipokuwa Dar es Salaam.”
Hasheem Thabeet Manka.
Haikuishia hapo kwani habari hiyo iliendelea: “Kwa macho yangu nilikuwa nikimuona huyo demu ambaye alikuwa Miss Tanzania ‘number’ 2 miaka michache iliyipota, akiwa na Hasheem kwenye kiwanja cha ‘Basketball’ cha Mlimani (UDSM), yaani demu alikuwa anamsubiri Hasheem hapo ‘basketball court’ karibia kila siku.Ikashibishwa zaidi: “Na kwa sasa dada huyo yupo Memphis, Marekani akiishi kama mke na mume na Hasheem Thabeet.”
Wakati tukisubiri udaku zaidi, habari hiyo ilimalizia: “Nimeipenda sana ‘couple’ yao sababu inaonekana ni mapenzi ya kweli, Hasheem katulia sana kwa sasa haoni wala hasikii juu ya huyo binti na binti na yeye kaacha shughuli zake Bongo kamfuata jamaa Marekani, binti pia ni msomi ndiyo kamaliza ‘University’ mwaka huu, alikuwa anasoma sheria pale Mlimani (UDSM).”
Baada ya mtandao huo kutoa maelezo hayo, Hasheem ‘alimcheki’ mmiliki wa mtandao wa Bongo Starlink, Dj Choka kupitia simu yake ya kiganjani usiku wa kuamkia Jumanne wiki hii ambapo alimwambia kuwa habari iliyosambazwa mtandaoni haina ukweli.
Alisema habari hiyo haikuwa na hata chembe ya ukweli licha ya kukiri kwamba kasikia Jokate yuko Marekani.
Jokate Mwegelo.
Choka aliandika: “Hasheem alinicheki kwa simu usiku wa leo (Jumatatu usiku) na kuniambia kuwa huyu mtu anayemiliki hiyo ‘website’ ni muongo kabisa.”.Kazi imefanywa na timu ya
No comments:
Post a Comment