header

nmb

nmb

Friday, October 8, 2010

DARFUR BADO HALI SI SHWALI!!

Mwanajeshi wa kulinda amani Darfur atekwa

KHARTOUM,Sudan

KIKOSI cha kulinda amani katika Jimbo la Darfur nchini Sudan kimesema kuwa mwanajeshi wake mmoja ametekwa nyara na wanamgambo wanaondesha mapigano katika eneo.

Tukio hilo ambalo limetokea katika mji wa El Fasher limekuja wakati ujumbe wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa unatembelea eneo hilo kutathmini shughuli za amani ya Darfur.

Kwa mujibu wa wanajeshi wa kulinda amani,mwanajeshi huyo alitekwa jana baada ya watu kadhaa waliojihami kwa silaha kuvamia nyumba ya wajumbe wa UNAMID.

Wamesema kuwa baada ya watu hao kuvamia nyumba hiyo, wanaume wawili walifungwa kwa kamba na wenzao wawili wakatekwa ambapo mmoja wa waliotekwa aliweza kutoroka baadaye lakini mwenzake hakufanikiwa.

Kumekuwa na matukio kadhaa ya raia wa kigeni kutekwa nyara tangu mahakama ya uhalifu ya kivita ya The Hague ilipotangaza kuwa Rais Omar Al Bashir anatakiwa kujibu mashtaka kadhaa ikiwa ni pamoja na mauaji ya kimbari jimboni Darfur na ukiukwaji wa haki za kibinadamu huku wengi ya wateka nyara wakiwa na nia ya kupata pesa.

Lakini utekwaji huu ambao umetokea katika mji ule ule wanaokaa wajumbe wa baraza la usalama,litatia wasiwasi mkubwa vikosi vya kulinda amani vya UNAMID.

Tayari wajumbe hao wa baraza la usalama hawajapata makaribisho ya kuridhisha kutoka kwa wale wanaomuunga mkono Rais Bashir,kufuatia baadhi ya wajumbe hao kukataa kukutana naye.

No comments:

Post a Comment