header

nmb

nmb

Friday, October 8, 2010

CHANZO CHA FOLENI MBEZI CHAJULIKANA !!


MADEREVA wa daladala zinazofanya safari zake kati ya Mbezi na Kariakoo, wameomba Askari wa Usalama wa Barabarani kuwepo katika kituo cha Mbezi Mwisho kila mara ili kuongoza magari kwa lengo la kuepuka msongamano.

Kituo hicho wamesema husababisha foleni kubwa kutokana na daladala zinazotoka mjini zinazoishia Mbezi kutaka kuingia kituoni hapo huku mabasi na malori mengine yanayotoka Kibamba na mikoani yakitaka kupita.

Kwa mujibu wa makondakta hao, eneo hilo kama hakuna trafiki, kunakuwa na foleni kubwa inayosababishwa na uzembe na ubishi wa madereva.

Mmoja wa madereva hao Musa Humari, akizungumza na gazeti hili amesema kuwa wamekuwa katika wakati mgumu wa kufanya biashara hiyo kutokana na foleni inayochangiwa na kuwepo kwa kituo hicho upande wa pili wa barabara.

Baadhi ya abiria wanaotumia kituo hicho wamedai kuwa foleni hiyo inaawathiri sana kutokana na kuwepo kwa magari makubwa na wanalazimika kuwahi kazini kwa kuwepo kituoni hapo kuanzia saa 10.30 alfajiri na wakati wakirejea nyumbani, mbali na foleni wanazokumbana nazo mjini, pia hukutana na foleni hiyo kuanzia Kibanda cha Mkaa hadi Mbezi.

Wameliomba Jeshi la Polisi kusimamia ipasavyo eneo hilo la kituo kwani ndiyo chanzo kikubwa cha foleni kwa vile kikoupande wa pili wa barabara kwa mabasi mengi yanayotoka mjini.kWA Habari kwa hisani ya gazeti la jioni la dar leo

No comments:

Post a Comment