header

nmb

nmb

Tuesday, October 12, 2010

BAADA YA KAIJANGE WA TFF KUVURUNDA MAMBO MBELE YA RAIS SERIKALI SASA YAPANDA MZUKA!!

NA MAGRETH KINABO- MAELEZO

SERIKALI imeiagiza Shirikisho ya Mpira wa Miguu Tanzania(TFF) kuhakikisha kuwa kuanzia sasa kila mchezo wa kimataifa unaofanyika hapa nchini ambao masharti yake ni kuimbwa nyimbo za Taifa kuwa zitaimbwa kwa ‘Brass

F) kuhakikisha kuwa kuanzia sasa kila mchezo wa kimataifa unaofanyika hapa nchini ambao masharti yake ni kuimbwa nyimbo za Taifa kuwa zitaimbwa kwa ‘Brass ban d’ kama ilivyokuwa inafanyika katika miaka ya nyuma.

Kauli hiyo ilitolewa jana (leo) na Waziri wa Habari, Utamaduni na Michezo Kapteni Mstaafu George Mkuchika katika hotuba yake iliyosomwa na Katibu Mkuu wa wizara hiyo Seth Kamuhanda wakati akizungumza na waaandishi wa habari jijini Dar es Salaam kuhusu tukio la kutoimbwa nyimbo za taifa za Morocco na Tanzania kabla ya mchezo wa kimataifa baina ya nchi hizo mbili uliofanyika Oktoba 9,mwaka huu kuanza.

Aliongeza kuwa hali hiyo ilisababisha adha kubwa kwa Rais Jakaya Kikwete aliyekuwa mgeni rasmi, washabiki, wapenzi wa soka, wageni na umma wa Tanzania kwa ujumla.

“Waziri ameielekeza TFF kuchukua hatua kali kwa yeyote atakayebainika kufanya uzembe na kulitia aibu kubwa taifa letu,” alisema Kamuhanda.

Aidha Katibu Mkuu huyo aliongeza kuwa uamuzi huo unalenga kuhakikisha kwamba aibu iliyotokea wakati wa mchezo huo, kuwa tukio la kutoimbwa kwa nyimbo za taifa halitokei tena

.

Akizungumzia kuhusu mitambo ya kuc hezesha CD iliyopo kwenye Uwa nja wa Taifa, Katibu Mkuu huyo alisema ni mizuri, safi na ni ya kisasa hivyo haina tatizo na watu wa kuiendesha wapo.

Katibu Mkuu huyo, Kamuhanda alisema jukumu la kufanya uchunguzi kuhusu tukio hilo ni la TFF wenyewe, hivyo wizara inaweza kushirikishwa kwa kutoa maelekezo na kuongeza kuwa wizara ndiyo imeelekezaTFF kufanya uchunguzi.

Kwa upande wake, Mkurugenzi wa Michezo, Leonard Thadeo, alisema wenye ujukumu la kufanya maandalizi ya kutosha kuhusu kupatikana kwa CD au kanda za nyimbo za taifa za timu husika ni TFF kama endapo timu inayokuja nyimbo yake haipo basi TFF huwasiliana nayo ilikuipata nyimbo hiyo.

No comments:

Post a Comment