header

nmb

nmb

Tuesday, September 7, 2010

OBAMA ATANGAZA MPANGO WA MABILIONI YA DOLA MAREKANI!!


Obama atangaza mpango wa mabilioni ya dolaWASHINGTON DC,Marekani
RAIS Barrack Obama ameelezea mpango wake wa miaka sita wa kuwekeza dola bilioni 50 nchini Marekani katika sekta za barabara, reli na katika njia za kukimbilia ndege.
Mpango huo ni moja wapo ya mipango ya kuichumi inayolenga kukuza ajira na kujaribu kuzuia chama chake cha Democratic kushindwa katika uchaguzi wa wabunge unaotarajiwa kufanyika mwezi Novemba mwaka huu.
Katika hotuba yake kwa wakazi wa Jimbo la Milwaukee, Rais Obama alisema kuwa atajenga maelfu ya kilometa za barabara kuu, reli na kukarabati mitambo ya usalama katika viwanja vya ndege na kwenye barabara.
Mpango huu wa Obama ni mojawapo ya nyenzo anazonuia kubuni nafasi za kazi na kujaribu kuzuia chama chake kupoteza ushswishi katika uchaguzi unatarajiwa wa Congress mwezi Novemba.
Wanasiasa wa chama cha Republican wamekosoa mpango huo na kusema hautafanikiwa na kuwa utaongeza gharama za matumizi ya fedha za serikali.

No comments:

Post a Comment