header

nmb

nmb

Tuesday, September 7, 2010

MTULIPE FIDIA YETU.RAIS WA LIBYA ,GADDAFI ALONGA!!


KIONGOZI wa Libya, Kanali Muammar Gaddafi, amesema Muungano wa Ulaya (EU)unapaswa kuilipa Libya takriban dola bilioni 6.3 kila mwaka ili kukomesha wahamiaji haramu Waafrika na kuepuka Ulaya nyeusi .
Akizungumza wakati wa ziara yake nchini Italia, Kanali Gaddafi alisema Ulaya inaweza kugeuka Afrika kwa kuwa kuna mamilioni ya Waafrika wanaotaka kuja.
Italia imeshutumiwa kwa kuwakabidhi Libya wahamiaji inaowakamata katika bahari yake kabla kwanza ya kuwachuja.
Matokeo yake ni kwamba wakimbizi wachache zaidi huwasili Italia kutokea Libya.
Takwimu za Muungano wa Ulaya zinaonyesha kuwa mwaka jana idadi ya watu waliokamatwa wakijaribu kuingia Italia kwa njia haramu ilipungua kufikia watu 7,300, kutoka 32,052 idadi ya mwaka 2008.
Kanali Gaddafi ameimarisha uhusiano wa karibu sana na Italia tangu kutia saini mkataba wa amani miaka miwili iliyopita uliokusudiwa kuondoa chuki za kihistoria kati ya Libya na Italia iliyokuwa mtawala wake wa kikoloni. .
"Kesho Ulaya huenda isiwe tena ya wazungu kwa kuwa kuna mamilioni ya wanaotaka kuingia. Hatujui kile kitakachotokea, hatujui wakristo wazungu watafanya nini watakapokabiliwa na mmiminiko huu wa Waafrika wajinga na wenye njaa, " alisema Kanali Gaddafi, aliyenukuliwa na Shirika la habari la Ufaransa AFP.
Alikuwa akizungumza katika sherehe za mjini Roma zilizohudhuriwa pia na Waziri Mkuu wa Italia, Silvio Berlusconi.
Ziara ya Kanali Gaddafi iligubikwa na hotuba yake nyingine iliyozusha ubishi mkubwa kwa vikundi viwili vya wanawake nchini Italia, ambao walilipwa euro 70 na 80 kila mmoja, akiwambia kwamba dini ya kiislamu inapaswa kuwa dini ya bara la Ulaya na kuwapa nakala za Quraan baada ya kuwahubiria kwa muda wa saa nzima kuhusu uhuru walio nao wanawake wa Libya.(BBC)

No comments:

Post a Comment