
Sheila asema hamuelewi Meryl
SHEILA na Meryl, wametumia muda mwingi pamoja katika jumba la Big Brother House, wamekuwa wakiongea na hata kulala pamoja.
Huku akiwa kakaa kwa raha mustarehe na Uti, sambamba na bia zao mkononi, Sheila, alianza kumteta Meryl.
Sheila, alisema Meryl ndiye mshiriki pekee ambaye hamuelewi katika jumba hilo.
Alisema, Meryl ni mtu ambaye anaweza kuchanganywa na vitu vidogo, Sheila alimwambia Uti kuwa hana uhakika na Meryl, na kwamba Meryl anataka kumchezea tu.
Sheila aliendelea kumwambia Uti kuwa, alikuwa akimjaribu Meryl mwisho wa wiki iliyopita, alimwambia Meryl kuwa Mwisho anampenda na kama angeweza angelala naye katika jumba hilo.
Sheila aliyasema haya kabla ya Mwisho na Meryl kupigana mabusu mbele yake.
No comments:
Post a Comment