
Kawe wacharuka* Wafanya maandamano usiku
*Wahoji ni Kipi au Angela ?
UBUNGO WAFANYA AJUA LEO BAADA YA KUTO PATIKANA MBABE!!
Christina Gauluhanga na Stella Aron, jijini
VISIKI vilivyoota katika Jimbo la Kawe na Jangwani imedaiwa kuwa, ndiyo vilivyosababisha maandamano yaliyofanywa jana na wananchi wa Kawe kupinga matokeo ya kura za maoni kwa upande wa Udiwani kwa tiketi ya Chama cha Mapinduzi (CCM).
Imedaiwa kuwa, wapo vigogo wenye majina yao ambao wamewakumbatia wagombea hao kila mmoja kwa nafasi yake wakijaribu kunyakua kata hizo maarufu nchini.
Kutokana na kuibuka kwa matokeo yenye utata ambapo kila pande iliyashtukia ilisababisha vurugu za maandamano kwa wana CCM hao huku wengine wakikimbia chama hicho na kuahidi kuamia upinzani ili waepukwe na kikombe cha rushwa na ufisadi.
Kwa upande wa Jimbo la Kawe, Kata yake ya Kawe kuliibuka vurumai ambapo kulitokea makundi mawili kila mmoja anamtaka mgombea wake.
Lipo kundi lililokuwa likimtaka Kipi Warioba huku wengine wakimtaka Angela Kiziga hali ambayo ilileta utata na kushutumiana kwa kila upande kuwa, wameiba kura.
Kutokana na hali hiyo kundi linalodaiwa kuwa, ni Warioba waliandamana kupinga matokeo ya ushindi huku wakitaka uchaguzi huo urudiwe.
Akizungumzia sakata hilo,Mecky Mbita ambaye ni Mwenyekiti wa Wazazi Tawi la Ukwamani amesema kuwa, wao ndiyo wanaojua ukweli wa matokeo halisi hivyo amewaomba wananchi kupunguza jazba na kufika kwenye vituo vya kura kwa ajili ya kupata ukweli wa matokeo hayo.
Kwa upande wa Kata ya Jangwani, kutokana na vurugu zilizojitokeza katika kura za uteuzi wa diwani wa kata hiyo, leo uchaguzi huo umerudiwa.
Wanachama wa kata hii wamegawanyika makundi mawili ambapo baadhi yao hawamtaki anayetetea nafasi hiyo huku wengine wakijipenyeza kwa ajili ya kulazimisha kushika kata hiyo ili waibuke kuwa washindi na kupata umeya.
Mmoja wa wagombea hao aliyeongea na gazeti hili, amesema kuwa, hizo ni njama za kisiasa hivyo raha ya kugombea ni kupata mshindi na atakayeshindwa akubali matokeo hivyo yeye amekomaa kisiasa na yupo tayari kwa matokeo yoyote.
Kule Jimbo la Kinondoni, hadi leo asubuhi matokeo ya Ubunge na Udiwani yalikuwa bado hayajatangazwa hali ambayo imezua utata kwa wanachama hao ambapo wanahisi kuwa huenda hujuma inataka kufanyika.
Hata hivyo matokeo hayo yaliahidiwa kutangazwa baadaye leo ambapo wananchi wamesema kuwa, endapo yasipotangazwa leo wapo tayari kuikacha CCM kwakuwa wamechoshwa na vitendo vyao vya kulazimisha ushindi.
Matokeo ya awali ambayo si rasmi tuliyoyapata wakati tukienda mtamboni imedaiwa kuwa, walioshinda kwa Upande wa Kawe ni Angela Kiziga, Ubungo ni aliyekuwa Mkuu wa Wilaya ya Bukombe, Hawa Ngumbi na Kinondoni na Idd Azzan.
No comments:
Post a Comment