BAADHI ya wanafunzi katika Shule ya Sekondari ya Wasichana ya Lugambwa mkoani Kagera wamezirai baada ya moto kuzuka ghafla na kuteketeza mali zao bwenini.
Moto huo uliozuka katika bweni lenye jina la Nyerere wakati wanafunzi wakiwa darasani, uliteketeza mali zote uliokuwa wakati wanafunzi hao.
Wakati moto huo unaaza ndani ya bweni hilo, kulikuwa na mwanafunzi mmoja aliyekuwa mgonjwa. Hata hivyo, aliokolewa na walinzi wa shule hiyo.
Kamanda wa Polisi mkoa huo, Henry Salewi, amesema tukio hilo limetokea jana saa 3 asubuhi wakati wanafunzi hao wakiendelea na masomo darasani.
Amesema baada ya wanafunzi na walimu kubaini kuwapo kwa moto huo kulitokea vurugu za wanafunzi kukimbia hovyo na wengine kuzirai baada ya kubaini kuungua kwa mali zao.
Moto huo ambao chanzo chake hakijajulikana haukusababisha madhara yoyote kwa binadamu.
No comments:
Post a Comment