header

nmb

nmb

Monday, August 23, 2010

Mkurugenzi wa Mazingira, Ofisi ya Makamu wa Rais Dkt. Julius Ningu akimkabidhi Dkt. Emmarold Mneney wa Taasisi ya kilimo Mikocheni ya jijini Dar es salaam kompyuta kwa ajili ya uimarishaji wa mtandao wa upashanaji na ubadilishanaji wa taarifa kuhusu viumbe, mazao na bidhaa ambazo vinasaba vyake vimefanyiwa mabadiliko ya kijenetiki leo jijini Dar es salaam ambapo Taasisi nne na Wizara mbili zimekabidhiwa vifaa hivyo vilivyogharimu jumla ya shilingi milioni 13.

Ofisi ya Makamu wa Rais imegawa kompyuta sita zitakazotumika katika upashanaji wa taarifa za masuala ya matumizi salama ya baiteknolojia ya kisasa kwa njia ya mtandao, kwa wizara na taasisi za serikali leo jijini Dar es Salaam.

Hayo yameelezwa leo na Mkurugenzi wa idara ya Mazingira kutoka Ofisi ya Makamu wa Rais, Dk Julius Ningu ambapo alisema kuwa, Tanzania ikiwa mojawapo ya nchi iliyoridhia itifaki ya Cartagena inayohusu Mazingira salama dhidi ya athari za Baiteknolija ya kisasa, ambayo inalenga zaidi kusimamia matumizi salama ya baiteknolojia ya kisasa, na vile vile ni njia muhimu ya kuboresha maisha ya binadamu hususan kwa kusimamia uzalishaji salama viwandani, chakula, kilimo na kuboresha afya ya binadam kwa ujumla.

Dk. Ningu ameeleza kuwa kompyuta hizo sita zimekabidhiwa kwa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi,Taasisi ya utafiti wa Kilimo ikocheni,Tume ya Taifa ya Sayansi na Teknolojia, Chuo Kikuu cha Dar es Salaam na Chuo Kikuu cha kilimo cha Sokoine (SUA).

Ameongeza kuwa Kompyuta hizo zimegharimu kiasi cha shilingi milioni kumi na mbili za Tanzania na mradi huo umetekelezwa chini ya ufadhili wa mfuko wa Mazingira wa Dunia kupitia Shirika la umoja wa mataifa linaloshugulikia mazingira (UNEP/GEF)

Habari hii imeandikwa na


Evelyn Mkokoi

Afisa Habari Ofisi ya makamu wa Rais

No comments:

Post a Comment