header

nmb

nmb

Wednesday, August 25, 2010

MIHEZOKWA WOTE KUHAMASISHWA NCHINI!!

Shirikisho la michezo kwa wote duniani (TAFISA) limeamua kushirikiana na serikali ya Tanzania kupitia chuo cha michezo cha Malya kilichopo mkoani Mwanza kwa lengo la kuimarisha michezo kwa wote nchini.

Akielezea juu ya ushirikiano huo kwa waandishi wa habari leo jijini Dar-es-salaam , katibu mkuu wa shirikisho hilo Bw. Wolfgang Baumann amesema shirikisho hilo linalowakilisha nchi kumi na tano duniani kote zikiwemo Japan na Australia linakusudia kushirikiana na wadau mbalimbali wa sekta ya Michezo nchini ili kuamsha Ari kwa watanzania kupenda michezo .

Hatua hiyo ya shirikisho inalenga kuimarisha afya,mwili na akili kwa Watanzania wa rika zote kuanzia watoto, vijana na wazee “ Shirikisho letu limeanzisha taasisi mpya zinakazoshughulikia maendeleo ya michezo kwa wote Afrika na maalumu kwa watu wazima ( Institute For Young Adults)

Baumann amesema shirikisho hilo linafanikisha shughuli zake duniani kote kwa msaada wa Umoja wa Mataifa kupitia kwa katibu wake mkuu bwana Ban-Ki-Moon ambaye amesaidia kwa kiasi kikubwa kuwezesha mpango wa michezo kwa wote duniani kufanikiwa.

Akielezea juu ya kuichagua Tanzania kuwa moja ya nchi za shirikisho hilo, Baumann alisema kwa muda mfupi waliotembelea maeneo mbalimbali wamefanikiwa kuona vipaji vya watanzania kupitia michezo tofauti licha ya kutokuwepo maeneo yenye viwango vya juu kimichezo.

Baumann amesema uamuzi wa kushirikiana na Tanzania utasaidia kuboresha sehemu za michezo hivyo kufanya watu wengi kujitokeza kushiriki kwa faida za afya,mwili na akili zao.

Kwa upande wake mtunza hazina wa Shirikisho hilo Bw. Brian Dixon amesema kuna umuhimu wa uimarishaji wa sekta ya michezo kutokana na mchango wake kwa maendeleo ya taifa huku akisisitiza kuwa ni vema watanzania wakajenga desturi ya kushiriki michezo mbalimbali kutokana na faida kubwa ikiwemo kuongeza umri wa kuishi duniani.

“ Nimepitia taarifa mbalimbali nikaona kuwa umri wa miaka ya kuishi kwa nchi za Afrika hauzidi miaka 50 tofauti na nchi za Ulaya na Magharibi ambapo wao huishi miaka 70 na kuendelea na hii ni kwa sababu wengi wanapenda kufanya mazoezi” Amesema.

Naye katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Utamaduni na Michezo Bw. Seith Kamuhanda amesema ujio wa viongozi hao wa TAFISA nchini Tanzania unalenga kuchochea maendeleo ya michezo na kuongeza kuwa serikali inaendelea kuboresha sekta ya michezo kwa kushirikiana na wadau mbalimbali na kupitia vituo mbalimbali vya michezo nchini kikiwemo chuo cha maendeleo ya Michezo Malya. Na wadau wa MAELEZO

No comments:

Post a Comment