header

nmb

nmb

Thursday, August 19, 2010

MAPAPARAZIIWATEMBELEA KAMBI YA MISS TANZANIA NA KUJIONEA MAKUBWA YA KAMBINI

Baadhi ya warembo wanaoshiriki katika shindano la Vodacom Miss Tanzania wakiwa katika picha ya pamoja leo kwenye kambi yao iliyopo kwenye hoteli ya Giraffe Ocean View Mbezi Beach kwa muda wa siku 28. Shindano la Vodacom Miss Tanzania linatarajiwa kufanyika mwezi Septema 2010 jijini Dar es salaam katika kutafuta mrembo wa Tanzania ambaye atawakilisha nchi kwenye shindano la Miss World hapo baadae mwaka huu. Leo ilikuwa ni siku ambayo imepangwa mahsusi kwa ajili ya warembo hao kukutana na wanahabari na kuongea nao mambo mbalimbali yanayohusu maandalizi kwa ajili ya shindano hilo kubwa nchini na linalodhaminiwa na kampuni ya simu za mikononi ya Vodacom Tanzania.
Hapa warembo wote wakipozi kwa picha ya pamoja wakati walipopigwa picha mbalimbali na wapiga picha wa vyombo mbalimbali vya habari. Kwa sasa wanahabari wameshuhudia nidhamu ya juu miongoni mwa warimbwendehao

No comments:

Post a Comment