header

nmb

nmb

Wednesday, August 4, 2010

MAKONGORO NAYE HATIHATI. NI BAADA YA VIGOGO WENGI CCM KUTUPWA NJE PATAHII.KATUNI YETU NI KWAN HISANI TYA DAR LEO!!


WAGOMBEA ubunge 11 wa Chama cha Mapinduzi (CCM) katika Jimbo la Segerea wamemwandikia barua Katibu Mkuu wa chama hicho, Yusuf Makamba, wakipinga ushindi wa mgombea Makongoro Mahanga wakidai kuwa kura zao zimechakachuliwa.

Wagombea hao wamefikia uamuzi huo baada ya kudaiwa kuwapo kwa wizi wa kura katika jimbo hilo na kusababisha ushindi usiokuwa halali ambapo wamedai kuwa pia wapo tayari kutinga hata mahakamani kudai haki zao.

Waliowasilisha rufaa hizo na kuomba chama kifanye tathimini ya matokeo ya awali yalioonesha Mahanga anang'ara ni pamoja na Joseph Kessy, John Jambele, Glorious Luoga, Zahoro Lihasaka na wenzao.

Pia kwa upande wa Temeke chama kimejikuta kikipokea idadi kubwa ya barua za rufaa muda mfupi baada na kabla ya kutangazwa kwa matokeo.

Hali hiyo iliyojitokeza na kujidhihirisha wazi wazi katika wilaya ya Temeke kwa idadi kubwa ya wagombea wa jimbo la Kigamboni kutokuwa na imani kutokana na mapungufu mengi yaliyojitokeza katika operesheni nzima ya kura za maoni.

Wanachama hao wamesema kulikuwa na mapungufu mengi ambayo yanapelekea wao kutokuwa na imani na matokeo hayo.

Walisema bahadhi ya mapungufu ni pamoja na kukamatwa kwa idadi kubwa ya kadi feki na uongozi kutoWachukulia Hatua wahusika licha baadhi ya makatibu kata kukiri kurubuniwa na wagombea.

Waliongeza kwa kusema kuwa kumekuwa na rafu za kupindukia hali inayopelekea matokeo ya mawakala na ya viongozi wa wilaya kutofautina.

Wagombea hao walisema kumekuwepo kwa idadi kubwa ya kura huku reja ya wanachama ikiwa na kura chache jambo ambalo mpaka sasa limezua kitendawili kisichoteguliwa.

Pia wanachama hao wameendelea kuhoji baadhi ya vituo kushindwa kutolewa matokeo hali inayoonyesha kuna ujanja unataka kufanyika wa kuwateuwa watu wanaowapenda baadhi ya watu.

Wakati huohuo, wananchi wamewalalamikia baadhi ya maofisa wa TAKUKURU kwa madai kuwa, wameshindwa kutekeleza majukumu ya kazi zao kwa kushindwa kuwanasa watuhumiwa wa rushwa ambao walikuwa wakimwaga fedha ovyo mitaani.

Wameongeza kuwa, watuhumiwa wengi walinaswa katika majimbo yote isipokuwa hali hiyo imeshindwa kutekelezwa kwa wananchi wa Temeke hali inayoonyesha kuna mkono wa mtu.

Wanachama hao wameomba watalaam mbalimbali kujitokeza kupima matokeo ya uchaguzi huo na kufanya tafiti mbalimbali za mazingira ya rushwa na kwa wagombea watakaokumbwa na kashfa hizo wapokonywe ushindi.

No comments:

Post a Comment