header

nmb

nmb

Monday, August 9, 2010

Konyagi wazindua kinywaji kipya Bismark Rocks chenye ladha ya nanasi (ABV 40%) uliofanyika Katika Jiji la Mwanza.

Meneja Mauzo wa Tanzania Distilleries Ltd ndugu Joseph Chibehe(kulia) akigonganisha glasi wakati wa sherehe za uzinduzi wa kinywaji hicho na mwakilishi wa wasambazaji wa bidhaa za Konyagi Kanda ya Ziwa ndugu Dilley Bhanji wa kampuni ya ALKA Traders.
Baadhi ya wafanyakazi wa Tanzania Distilleries ltd waliowawakilisha wenzao wakiwa katika picha ya pamoja katika uzinduzi huo.

Mwaigo- Kanda ya kaskazini Mashariki (kushoto), Resty mama wa kudhibiti mshiko na Mwesi- Kanda ya Kusini, wakimhakikishia mama mdhibiti mshiko wa kampuni kwamba wana uhakika kuwa wataalamu wa uzalishaji kiwandani walizingatia kwa kiwango cha juu kikudhi mahitaji ya wateja, hivyo basi asiwe na shaka mauzo yatakuwepo na wateja wamethibitisha kwa kufurahia kinywaji Bismark Rocks chenye ladha ya Nanasi na kilevi 40%.



Warembo wa Tanzania Distilleries Ltd wakiwa wanaonesha Bismark Rocks yenye ladha ya nanasi kwa wateja na wewe unaye angalia sasa hivi.


Wasanii wakiwatumbuiza wateja wakati wa uzinduzi huo.
Imetayarishwa na Mdau wetu Narcisius Ngaillo -Mazoo!

No comments:

Post a Comment