header

nmb

nmb

Thursday, July 1, 2010

YADAIWA JIMAMA LAMUWEKA KINYUMA MSANII WA LUNINGA NI DR. CHENI!!


Nyota wa filamu Bongo, Mahsein Awadh ‘Dokta Cheni’, ameingia katika orodha ya wasanii waliowahi kukanyaga skandali baada ya madai ya hivi karibuni kuwa, ‘analelewa’ na jimama lenye ‘mapene’ ambaye makazi yake yapo Upanga, jijini Dar.
Amani ‘news paper’ ndiyo liko kifua mbele kuianika ishu nzima, baada ya kupata kutoka kwa chanzo chake makini.
Kikiongea kwa kujiamini, chanzo hicho kilidai kuwa, jimama hilo limemfanyia mambo makubwa Dokta Cheni ikiwa ni pamoja na kumnunulia ‘mkoko’ (gari) kitendo ambacho kinaelekea kuyumbisha ndoa yake ambayo haijafikisha nusu mwongo mmoja tangu kufungwa.
Kiliendelea kusema kwamba, Cheni kwa sasa anakuja juu kutokana na pesa za jimama hilo ambalo halina mume wala mchumba, achilia mbali buzi.
“Cheni anaonekana kujisahau kabisa kwani ameridhishwa na jimama ambalo haliendani kabisa na mke wake,” kilisema chanzo hicho.
Kufuatia data zote hizo Amani lilimnyooshea ‘waya’ Dokta Cheni na kumsomea mashtaka yake ambapo baada ya kumtajia jina la jimama hilo alikiri kumfahamu, lakini akadai kuwa, ni mtu wanayeshirikiana katika kazi kwa ukaribu zaidi tofauti na watu wanavyoamini.
Cheni aliendelea kuweka wazi kwamba, kazi anazofanya yeye na mwanamke huyo ni kuingiza magari nchini Tanzania na kuuza kupitia kampuni ya jimama hilo.
Aidha, msanii huyo ambaye anataka kutoka na filamu yake mpya hivi karibuni, alisema mbali na magari, walikuwa katika mchakato wa kuingiza umeme unaotokana na Taka ambao ungefanywa na warabu waliotarajia kutua nchini kabla ya mpango huo kusitishwa.
“Unajua wabongo ndiyo maana hawaendelei kamwe, kwani kazi ni kupiga majungu tu, hasa wanapomwona mtu anaendelea, hayo maneno hayanishtui kwani yamesemwa siku nyingi ni nyie mlikuwa hamjasikia, kwani mtu hawezi kufanya kazi kwa karibu na mwanamke mpaka awe mpenzi wake?
“Mbona hawanisifii kuwa, nimecheza filamu nzuri ya kutisha na inatoka mtaani wiki ijayo wanasema mambo yasiyokuwa na maana,” alihoji Cheni.
Cheni alimalizia kwa kusema kuwa, anachoangalia yeye ni maendeleo zaidi na ndiyo maana amejikita zaidi katika filamu na yule atakayemsaidia, awe mwanamke au mwanaume hatoogopa kuwa naye karibu.
“Kwa sasa naangalia maendeleo zaidi kwani natarajia kuwa juu kwasababu nimetoa filamu yangu ya One By One ambayo itaanza kutoka rasmi mtaani Jumatatu ijayo,” alisema

No comments:

Post a Comment