header

nmb

nmb

Thursday, July 1, 2010

Sudan yamuachia Huru mpinzani!!


Sudan yamuachia mpinzaniKHARTOUM,Sudan
MSAIDIZI wa kiongozi wa upinzani nchini Sudan, amesema kuwa Serikali ya nchi hiyo imemuachia huru kiongozi huyo, Hassan al-Turabi ambaye ilikuwa ikimshikilia kwa muda wa miezi kadhaa.
Msaidizi huyo amesema kuwa Turabi aliachiwa kutoka mahabusu jana baada ya kutumia muda wa mwezi mmoja na nusu tangu alipokamatwa na Serikali mwezi Mei mwaka huu na kisha kulifungia gazeti lake la chama.
Mkewe alisema kuwa kiongozi huyo alikamatwa baada ya kurudia tena kauli yake ya kusema kuwa uchaguzi mkuu uliofanyika nchini humo na Omar al-Bashir kuchaguliwa tena ulijaa hujuma.
Mpinzani huyo ambaye ni kiongozi wa kidini alisema kuwa uchaguzi huo wa kwanza wa vyama vingi tangu mwaka 1986 ulijaa hujuma na mapungufu mengi.
"Turabi amekwishawasili nyumbani kwake lakini hatufahamu ni kwanini ameachiwa ,"msaidizi wake huyo Awad Babiker ameliambia Shirika la Habari la Uingereza, Reuters.
Turabi, ambaye ni mshirika mkuu wa zamani wa rais amekwishakamatwa mara kadhaa tangu alipoanzisha chama chake cha Popular Congress.BBC

No comments:

Post a Comment