habari
MAOFISA wa Serikali ya Uganda wamesema vikosi vya wanausalama vimefanikiwa kupata mkanda unaotumiwa na walipuaji wa mabomu ya kujitoa mhanga ambao haujalipuka katika eneo la ambalo lilitokea shambulizi katika mji wa Kampala Jumapili iliyopita na kusababisha vifo vya watu waliokuwa wakitazama fainali ya Kombe la Dunia kupitia televisheni.
Maofisa hao walisema jana kuwa mbali na mkanda huo, kuna idadi ya watu ambao haijajulikana wamekamatwa.
Mataifa ya watu hao waliokamatwa hayajatajwa lakini maofisa wamesema kichwa kimoja kilichopatikana karibu na eneo moja ulipotokea mlipuko huo kinaonekana kuwa cha raia wa Somalia ambaye huenda alikuwa amejitoa mhanga.
Takriban watu 74 waliuawa katika milipuko miwili iliyotokea katika klabu ya Raga na kwenye mgahawa.
Kundi la wapiganaji la Kisomali la al-Shabab tayari limetamka kuhusika na mashambulio hayo kwa kile linachodai ni kutokana na Uganda kuunga mkono Serikali ya Somalia mjini Mogadishu.
Msemaji wa serikali, Fred Opolot, amesema ukamataji ulifanyika baada ya Mkanda huo kukutwa katika eneo la Makindye Kusini Mashariki mwa Kampala.
Polisi wamesema, mkanda huo ulikutwa kwenye mfuko mweusi kama ule unaotumika kubebea kompyuta aina ya lap-top kwenye klabu ya usiku Jumatatu mchana.
Kutokana na tukio Polisi wa Uganda wanasaidiwa na wachunguzi kutoka Marekani wakijaribu kutambua namna hasa ya milipuko hiyo ilivyopangwa na kulipuliwa.
Mwandishi wa Shirika la Utangazaji la Uingereza (BBC) anayeshughulikia masuala ya Afrika Mashariki, Will Ross, amesema serikali ya Uganda iko katika shinikizo kubwa kuonyesha kuwa inaweza kuzuia tukio hilo la milipuko kama hiyo kutokea tena.
Katika hatua nyingine, Umoja wa Afrika (AU), ambao umepeleka majeshi yake ya kulinda amani nchini Somalia, unatarajiwa kufanya mkutano mjini Kampala baadaye mwezi huu na maofisa wamesema utafanyika kama ulivyokuwa umepangwa.
Taarifa hiyo imekuja wakati Uganda imeanza maombolezo ya kitaifa ya siku saba, huku bendera zikishushwa nusu mlingoti kote nchini huku wanamgambo mjini Mogadishu msemaji wa al-Qaeda anayeshirikiana na kundi la al-Shabab, Sheikh Ali Mohamud Rage, akitishia kufanya mashambulizi zaidi nchini humo.
Katika taarifa ya kionmgozi aliyoitoa juzi alisema kuwa Al-Shabab wamehusika na milipuko hiyo miwili Uganda huku akisema kuwa miji ya Uganda naBujumbula itaendelea kuandamwa na milipko endapo Serikari ya za nchi hizo mbili hazitawaondoa wanajeshi wake nchini Somalia.
Waandishi wamesema idara za usalama eneo hilo sasa zitakuwa zinatathmini upya namna ya kujilinda kutoka jeshi lililothibitisha kuwa na nia na uwezo wa kushambulia nje ya mipaka ya Somalia.
Kutokana na hali hiyo,Serikali ya Kenya imesema imeimarisha usalama katika mpaka wa nchi hiyo na Somalia.
Kenya ni washirika wa karibu na serikali ya Somalia na inawasaidia kutoa mafunzo ya kijeshi.

No comments:
Post a Comment