header

nmb

nmb

Wednesday, July 14, 2010

MTETEA HAKI ZA BINADAM WA TANZANIA NAYE AUWAWA KWA RISASI KAMAYULE WA KONGO!!


KUNDI la watu wanaodhaniwa kuwa majambazi, wakiwa na silaha, wamevamia nyumbani kwa Profesa Juan Mwaikusa (58) wa Kitivo cha Sheria kutoka Chuo Kikuu cha Dar es Salaam na mkazi wa Salasala, kisha kumpiga risasi kifuani na kuwauwa wengine wawili waliokuwa wakimsadia, akiwamo mtoto wake.

Kwa mujibu wa mashuhuda wetu, tukio hilo limetokea jana saa 4 usiku wa kuamkia leo nyumbani kwake, Mbezi Salasala.

Imedaiwa kuwa majambazi hao walimvizia profesa huyo nje ya nyumba yake wakati akitoka kwenye mihangaiko yake na mara baada ya kufika walilizingira gari lake kisha kuanza kumfyatulia risasi.

Kutokana na vurumai hizo, watoto wake waliokuwa ndani wakiangalia televisheni walisikia mlio kama wa pancha, ndipo walipotoka kuangalia na waliwaona majambazi hao wakiwa wamemuelekezea bunduki kifuani profesa huyo.

Kuona hivyo, watoto hao walirudi mbio ndani kisha kupiga simu polisi ambapo baada ya muda mfupi walianza kusikia milio ya risasi mfululizo.

Shuhuda wetu amedai kuwa vurumai hiyo ilisababisha mtoto Gwamaka Daud (25), na jirani yao, John Mtui (40-45), kuanza kushambuliana na majambazi hao.

Kwa bahati mbaya majambazi hao walifanikiwa kuwauawa profesa huyo na waliokuwa wakimsaidia.

Kaimu Kamanda wa Polisi Kanda Maalum Dar es Salaam, Charles Kenyela, amethibitisha kutokea kwa tukio hilo ambalo anadhani kuwa ni la kulipiza kisasi.

Amesema watu hao walifanya unyama huo ambapo walifika katika nyumba hiyo wakiwa na pikipiki kisha kutoweka bila kupora kitu chochote.

“Jeshi langu linajipanga kuhusiana na mauaji haya ya kikatili na nina imani kuwa tutawatia mbaroni wahusika wote,” amesema Kamanda Kenyela.

Mwenyekiti wa Chama Cha Tanzania Labour Party (TLP), Augustino Mrema, amesema chama chake kimesikitishwa na kifo hicho na kuiomba Serikali kufanya uchunguzi wa kina ili kuweza kutambua chanzo cha mauaji hayo.

“Hii inatishia amani sasa. Tunaiomba Serikali ifanye uchunguzi ili iweze kubaini wahusika kwani hivi sasa kumekuwa na matukio ya mauaji ya watu wasio na hatia,” amesema Mrema.

Mrema amesema kifo cha Mtui, ambaye ni jirani aliyekwenda kumsaidia Profesa Mwaikusa, kimemsikitisha sana kwa sababu alikuwa ni rafiki yake wa karibu.
Dar leo ya Leo

No comments:

Post a Comment