header

nmb

nmb

Thursday, June 24, 2010

WIZI NINOMA NJEMBA YATUPWA LUPANGO!!

JOHN Deus (18), mkazi wa Vingunguti, amehukumiwa kifungo cha mwaka mmoja jela baada ya kupatikana na hatia ya kuiba mali za mama yake mzazi.
Mshitakiwa amesomewa hukumu yake na hakimu Emanuel Mbonamasabo wa Mahakama ya Mwanzo Buguruni.
Hakimu alidai kutokana na maelezo ya mlalamikaji Pole Kassim ambaye ni mama mzazi wa mshitakiwa pamoja na ushaidi kutoka pande zote mbili ulionyesha kuwa, mshitakiwa ni kibaka sugu kwani mara kwa mara alikuwa akiiba mali za mama yake na majirani na kuziuza.
Ambapo Machi 28, mwaka huu, saa 3 usiku, Vingunguti Miembeni mshitakiwa aliamua kuiba deki moja yenye thamani ya sh.45,000, simu aina ya Zantel yenye thamani ya sh. 30,000 na fedha tasilimu sh.105,000 mali ya mlalamikaji.
Aidha mshitakiwa alipopewa nafasi ya kujitetea mbele ya Mahakama ili asipewe adhabu kali, aliiomba mahakamaimpunguzie adhabu kwa kuwa ni mgonjwa wa UKIMWI.
Mshitakiwa alipotakiwa kutoa kadi ya Hospitali inayoonyesha ana muathirika hakuweza kufanya hivyo nakuonekana wazi kuwa alikuwa akiidanganya mahakama.
Hata hivyo, hakimu aliamua kumtia hatiani na kumhukumu kifungo cha mwezi mmoja jela mshitakiwa Patrick Dickson (28), mkazi wa Buguruni, kutokana na kuhusika kununua mali za wizi kutoka kwa John Deus ambaye ni mshitakiwa namba moja.
Alidai kuwa katika shitaka hilo la wizi mshitakiwa Dickson aliusika kununua deki iliyoibiwa na Deus ambayo ilipatikana katika chumba chake.
Dickson alipopewa nafasi ya kujitetea ili asipewe adhabu kali alidai kuwa aliiomba mahakama isimpe adhabu kali kwani hilo ni kosa lake la kwanza na hakujua kama deki hiyo ilikuwa ni ya wizi.
Awali karani wa Mahakama hiyo Hyasinta Mambo alidai kuwa Machi 28, mwaka huu, saa 3 usiku, Vingunguti Miembeni mshitakiwa John Deus aliiba deki moja yenye thamani ya sh. 45,000, simu aina ya Zantel yenye thamani ya sh. 30,000 na fedha tasilimu sh. 105,000 mali ya Pole Kassim.

No comments:

Post a Comment