KESI inayomkabili Mtangazaji wa Kituo cha Televisheni ya Taifa (TBC), Jerry Muro, leo imeanza kuunguruma katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu.
Mshtakiwa huyo pamoja na wenzake wamesomewa maelezo ya awali na katika mashtaka ya kuomba rushwa ya sh. milioni 10 .
Washitakiwa wengine katika kesi hiyo ni Edmund Kapama na Deogratius Mgasa ambapo kesi hiyo ipo mbele ya Hakimu Gabriel Mirumbe wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu.
Katika shitaka la kwanza ilidaiwa kuwa washitakiwa wote kwa pamoja walikula njama, waliomba rushwa, na shitaka la tatu ni kwa mshitakiwa wa pili na watatu ambao wao walijipachika wadhifa usio wao na kuomba rushwa.
Ilidaiwa kuwa Januari 29, mwaka huu, wakiwa katika Hoteli ya Sea Cliff, washitakiwa waliomba rushwa kutoka kwa Wage ili habari zake kuhusu ubadhirifu zisitangazwe kwenye kituo cha televisheni cha TBC1.
Washtakiwa hao wamekana mashtaka na kesi hiyo itaanza kusikilizwa Julai 17 mwaka huu na upande wa mashitaka una mashaidi 11.
No comments:
Post a Comment