MKUU wa Mkoa wa Dar es Salaam, William Lukuvi, amesema anasikitishwa kwa Jiji la Dar es Salaam kuongoza kwa kuwa na magari ya kubeba taka ambayo mabovu na ambayo hayatakiwi duniani
Amesema kuwa jiji la Dar es Salaam limegubikwa na uchafu katika maeneo mbalimbali ya jiji huku magari yanayozoa taka yakiedelea kutembea barabarani bila kuchukuliwa hatua.
“Magari ya kuzoa taka ni mabovu lakini nashangaa yanaachiwa yakiendelea kutembea barabarani na kusamahewa,” amesema.
Amesema mbali ya kuwapo kwa magari hayo mabovu, pia usimamizi wa uzoaji taka ni mbovu kwani kila sehemu kuna dampo la uchafu.
Amesema kero hiyo inatokana na kuwapo kwa baadhi ya watu kupenda fedha badala ya kujali kazi na kusababisha kuendelea kwa kero hiyo.
“Wapo wanaofanya vizuri na wengine vibaya. Kama ningekuwa na jela mimi ningewafunga kutokana na kuendelea kwa hali mbaya ya jiji. Hii ni hatari sana,” amesema Lukuvi.
Amesema kutokana na kuchoshwa na hali hiyo sasa ameazimia kufanya ziara katika kata tano ambazo zimeonekana kuwa ni sugu kwa kuzagaa kwa uchafu na hatua kali zitachukuwa kwa wahusika.

No comments:
Post a Comment