header

nmb

nmb

Tuesday, May 4, 2010

WAMBURA WENZAKE KUFUTWA UANACHAMA, NI KWA KITENDO CHA KWENDA MAHAKAMANI!!

Katibu Mkuu wa TFF F. Fredirick Mwakalebela kushoto na Frolian Kaijage Msemaji wa TFF wakizunumza na waandishi wa habari leo.

Katibu mkuu wa TFF kushoto Fredirick Mwakalebela pamoja na msemaji wa shirikisho hilo Frolian Kaijage wamezungumzania mgogoro wa wanachama wa Simba kwenda mahakamani katika mkutano na waandishi wa habari kuhusiana na katiba ya FIFA inasemaje iwapo masuala ya michezo yatapelekwa katika mahakama za kawaida.

Jumapili Mei mbili mwaka huu TFF ilitoa taarifa kwa vyombo vya habari kwamba kwa mujibu wa katiba ya FIFA utatuzi wa migogoro ya kimichezo hairuhusiwi kamwe kupelekwa katika mahakama za kawaida za nchini ,
Pia TFF kama mwanachama wa FIFA inawajibika kutimiza wajibu huu chini ya ibara 13 (1) (D) .Wajibu huu unaihusu TFF na wanachama wake kama ilivyoainishwa katika katiba ya TFF Ibara ya 1 6.

Katiba hiyo ilielezwa kuwa TFF inawajibika kuheshimu maagizo,kanuni,katiba na maamuzi ya FIFA.

Hivyo TFF inawaeleza tena wanachama wake wakiwemo SIMBA SPORTS CLUB kwamba ni marufuku kupeleza migogoro ya kimichezo katika mahakama za kawaida za nchi kwa kufanya hivyo kutasababisha wanachama kufukuzwa uanachama wake.pamoja na kuifutia uwanachama klabu ya SIMBA kutoshiriki mashindano ya ndani na nje ya nchi
Hivyo TFF imeutaka uongozi wa Simba kuwachukulia hatua wanachama wake kutokana na kitendo hicho cha kwenda mahakamani kwani kufanya hivyo wanakiuka katiba yao wenyewe kanuni

No comments:

Post a Comment