header

nmb

nmb

Wednesday, May 5, 2010

WAKATI TFF YAAGIZA WAMBURA NA WENZAKE WAFUKUZWE UANACHAMA YEYE AFUNGUA KESI MAHAKAMA MBILI IMEFAHAMIKA LEO!!

WAMBURA AKIZUNGUMZA NA VYOMBO VYAHABARI

Michael Wambura aliyekuwa mgombea uenyekiti wa klabu ya Simba akizungumza na waandishi wa habari leo kwenye ukumbi wa Idara ya Habari Malelezo juu ya kufungua kesi katika mahakama mbili Mahakama kuu na mahakama ya Kisutu.

Amesema Katiba ya Simba imekiukwa kwani Simba ilitakiwa kuunda kamati ya Rufaa ambayo ndiyo ingekuwa na mamlaka ya kushughulikia matatizo ya Simba juu ya uchaguzi.
Amsema kamati hiyo pamoja na kamati ya Uchaguzi iliyopo sasa zilitakiwa kupewa baraka ama kuthibitishwa na kamati ya utendaji ya Simba kitu ambacho hakijafanyika hivyo hata kamati ya uchaguzi ya Simba ya sasa ni Batili kwa mujibu wa katiba ya Simba.

Wambura amesema wamefungua kesi mbili katika Mahakama Kuu na Mahakama ya Kisutu ili kutafuta haki.

Anasema kwa kutolea mfano wa hukumu moja iliyowahi kutolewa na Jaji Bubeshi wa mahakama kuu ya mwaka 1996 iliyokuwa ikimkabili Muhidin Ndolanga na Baraza la Michezo.

Akinukuu moja ya kifungu katika hukumu hiyo Wambura anasema "kifungu hicho kilieleza kwamba kama unanyang'anywa haki usingoje muda upite itafute hata mahakamani kwa kipengele hicho, anasema mahakama imemruhusu kutafuta haki yake huko, lakini pia anasema kwa kuwa katiba ya Simba inatambua Katiba ya Jamhuri ya muungano wa Tanzania hivyo imeruhusu mwanachama yeyote kwenda mahakamani kudai haki yake".
Ameongeza kwamba ameliarifu Shirikisho la Soka Afrika CAF na Shirikisho la Soka la Dunia FIFA kuwa kuna mgogoro katika klabu ya Simba na TFF hivyo amekwenda mahakamani kudai haki yake. By prhabari.

No comments:

Post a Comment