header

nmb

nmb

Saturday, May 8, 2010

PAPA AMTEUWA Padre Gabriele Ferdinando Bentoglio,kuwa katibu Mkuu!!
BABA Mtakatifu Benedikto wa kumi na sita, amemteua mheshimiwa Padre Gabriele Ferdinando Bentoglio, kuwa Katibu mkuu msaidizi, Baraza la Kipapa la wahamiaji na watu wasiokuwa na makazi.
Kwa mujibu wa taarifa kutoka Vaticana,Katibu mkuu mteule anachukua nafasi iliyoachwa wazi na Askofu mkuu Novatus Rugambwa aliyeteuliwa na hatimaye kuwekwa wakfu kuwa Askofu mkuu na Balozi mpya wa Vatican nchini Angola, Sao Tome na Principe.

Aidha taarifa hiyo imesema kuwa Padre Gabriele kabla ya kuteuliwa alikuwa Katibu Mkuu wa Shirika la Wamissionari wa Mtakatifu Carlo, maarufu kama Waskalabriani. By Thomson Mpanji Mbeya

No comments:

Post a Comment