header

nmb

nmb

Wednesday, May 19, 2010

MISIMA YA MAJONZI MJINI MOROGORO!!


WATU wawili wamefariki dunia mkoani Morogoro katika matukio mawili tofauti likiwemo la mmoja kukutwa amekufa kwenye mto Ngerengere huku mwili wake ukiwa hauna majereha.
Kwa mujibu wa Kamanda wa Polisi Mkoa wa Morogoro Bw. Thobias Andengenye alisema tukio hilo lilitokea juzi katika maeneo ya Chamwino Manispaa ya Morogoro.
Kamanda Andengenye alisema kuwa kutokana na matukio hayo upelelezi unafanyika ili kubaini kifo cha Fikiri Juma(24)mkazi wa Chamwino mjini ambaye mwili wake ulikutwa ukiwa ndani ya mto Ngerengere maeneo ya Kasanga huku ukiwa umefungwa kitambaa usoni na mikononi.
Katika tukio jingine lilitokea wiki iliyopita katika maeneo ya Ifakara, mwili wa marehemu ambaye hakuweza kufahamika mara moja ulikutwa barabarani.
Akizungumzia tukio hilo Kamanda Andengenye alisema kuwa tukio hilo lilitokea katika maeneo hayo na mwili huo ulikuwa na majeraha.
Hata hivyo chanzo cha tukio hilo bado hakijafahamika ,huku upelelezi zaidi kuhusiana na tukio hilo ukiendelea.

No comments:

Post a Comment