header

nmb

nmb

Wednesday, May 19, 2010

Mama huyu angekufa katika kisima cha maji!!Na Mwajuma Juma, Zanzibar
MKAZI wa Kisuauni Wilaya ya Magharibi Unguja, Bi. Zuwena Khamis Rashid (26) amenusurika kufa baada ya kutumbukia kwenye kisima.
Tukio hilo lilitokea juzi nyakati za mchana ambapo aliokolewa na raia wema walioshirikiana na Kikosi cha Zimamoto na Uokozi (KZU).

Kwa mujibu wa Kamanda Aziz, alisema mara baada ya kuokolewa alipelekwa katika Hospitali Kuu ya Mnazimmoja kwa ajili ya matibabu zaidi ambapo uchunguzi wa awali uliofanyika ulibaini kuwa na matatizo ya akili.
Hata hivyo anaendelea kupatiwa matibabu katika hospitali hiyo na hali yake inaendelea vizuri.

Aidha Kamanda huyo alitoa wito kwa wananchi wanaokaa na watu wenye matatizo ya akili wakiwemo watoto wadogo kuwa waangalifu kwa kuwatunza ili kuwanusuru na majanga kama hayo.

Alisema jamii inapaswa kufahamu kwamba watu wenye matatizo ya akili wanapaswa kulindwa kwa hali zote kwani kuwaachia huru kutawasababishia hatari ama kupoteza maisha yao

No comments:

Post a Comment