header

nmb

nmb

Saturday, May 1, 2010

MATUKIO YA KUTUPA WATOTO YAENDELEA KWA KASI. HII YA MKOANI RUKWA!!

Kichanga cha kike kikiokotwa na Polisi kanzu baada ya kutupwa na mamayake DSM.
HABARI YA RUKWA

POLISI mkoani Rukwa inamshikilia mwanafunzi wa Chuo cha Elimu ya Taifa Rukwa kwa tuhuma za kujifungua mtoto wa kike na kutelekeza kichanga kando ya Mto Manzintwise na kusababisha kifo cha mtoto huyo. Taarifa zilizopatikana katika eneo hilo na kuthibitishwa na polisi zimemtaja mtuhumiwa huyo kuwa ni Frola Kakwaya (22), mwanafunzi wamwaka wa pili katika chuo hicho.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Rukwa, Bw. Isunto Mantage alisema kuwa mwanafunzi huyo aligunduliwa na majirani zake kuwa ni mjamzito, lakini muda wa kujifungua ulipotimia walishangaa kuona hana ujauzito, ndipo walimfuata na kumuuliza imekuwaje, na aliposhindwa kuwajibu wakaamua kutoa taarifa polisi.
Kamanda huyo alisema baada ya polisi kumkamata walimpeleka hospitali na kubainika kweli alijifungua, na alipohojiwa alipokiri kujifungua mtoto wa kike akiwa hai, na kumtelekeza kando ya Mto Manzitwise katika Kitongoji cha Izia, Manispaa ya Sumbawanga.
Polisi walipofika katika eneo hilo hawakukuta kichanga hicho, lakini siku iliyofuata, watoto wakiwa wanacheza kwa kujifunza kuvua samaki waliopoa kitu kizito kikiwa kimeviringishwa na upande wa kanga, na mara baada ya kukifungua waligundua kuwa ni mwili wa mtoto mchanga na kutoa taarifa kwa majirani ambao pia walitoa taarifa katika kituo cha polisi.
Kwa mujibu wa Kamanda Mantage uchunguzi wa kitabibu umebaini kuwa mtoto huyo alifariki dunia kutokana na baridi na kukosa uangalizi wa kutosha.
Mtuhumiwa huyo atapandishwa kizimbani mara baada ya upelelezi hilo kukamilika.
Juddy Ngonyani, Rukwa

No comments:

Post a Comment