header

nmb

nmb

Wednesday, May 5, 2010

Katibu kanisa Katoliki Mbeya afariki baada ya kusoma risala ya ufunguzi wa hotel...!

Askofu Chengula

KANISA Katoliki limewataka Wanawake kuteteta haki zao za msingi kwa kukemea na kuhakikisha wanakomesha vitendo viovu vya utoaji mimba na kuuwa watoto.

Aidha kanisa hilo limetoa mwito kwa wanawake hao kuwa mstari wa mbele katika shughuli mbalimbali za kiroho,kiuchumi na kijamii na kuwa mfano wa tunu bora ya kanisa katika kuendelea kulijenga kanisa kwa kuwaandaa vijana katika misingi imara ya maadili mema kiroho na kimwili.

Hayo yamesemwa na Askofu Evaristo Chengula katika mafundisho ya Wanawake Wakatoliki Tanzania (WAWATA),Jimbo la Mbeya wakati wa hafla fupi ya kuzindua mradi wa hoteli ya jimbo,maeneo ya Forest ya zamani,jijini Mbeya.

Askofu Chengula alisema wanawake wakatoliki Tanzania (WAWATA),Jimbo la Mbeya wana jukumu kubwa la kuhakikisha kanisa linaendelea kuwa kisima cha hekima na busara,amani,utulivu,haki,upendo na mshikamano.

Alisema chama hicho ndicho chombo pekee cha kuwajenga wakatoliki kuishi katika misingi ya utu na haki pamoja na kuwaandaa vijana kuwa watumishi waaminifu na wanyenyekevu katika shughuli za utume katika kanisa na jamii kwa ujumla.

“Kina mama wakatoliki nyie ndiyo walezi wa kanisa,hakikisheni mnasiamam imara katika kukemea vitendo viovu vya utoaji wa mimba na kuuwa watoto wasio na hatia,wajengeni vijana katika maadili mema ili waweze kuitwa katika miito mitakatifu,”alisema.

Kwa upande wake,Katibu wa wawata Jimbo,Annamaria makombe akisoma risala mbele ya Askofu alisema kuwa zaidi y ash.Mil.10 zimetumika katika kukamilisha ujenzi wa jengo la hoteli lililoshirikisha akimama wa Parokia zote 30 za jimbo la Mbeya.

Wakati huo huo,Katika hali iliyowashtusha na kuwasikitisha waumini wa Kanisa katoliki, ni kutokea kwa kifo cha Katibu wa Wawata,Jimbo,Makombe ambaye alikuwa msoma risala siku ya ufunguzi wa Hoteli hiyo.

Kwa mujibu wa Mwenyekiti wa WAWATA Jimbo,Christina Mtengule marehemu alifariki dunia akiwa usingizini usiku wa kuamkia jana baada ya kumaliza sherehe za uzinduzi wa hoteli na kuagana vizuri kwa furaha,Bwana ametoa na ametwaa,mwenyezi mungu aiweke roho ya marehemu Makombe peponi amina.

Thanx Mpanji, Mbeya

No comments:

Post a Comment