header

nmb

nmb

Wednesday, May 5, 2010

JAKAYA PONGEZWA KWA KUWA KIDETE NA MALARIA!!

Benjamin Sawe -Maelezo Dar es SalaamRais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Jakaya Kikwete amesema Serikali ya Tanzania inafanya kila jitiada za kupambana na ugoonjwa hatari wa Malaria.Rais Kikwete amesema jitiada hizo ni pamoja na kunyunyuzia dawa katika mazalia ya mbu,kuhamasisha utumiaji wa neti,ikiwa ni pamoja na matumizi ya dawa mseto.

Alisema kwa Tanzania ugonjwa wa Malaria ni ugonjwa namba moja unaosumbua jamii hivyo serikali ya Tanzania imehakikisha njia hizo tatu za kupambana na malaria zinatumika kwa uhakika ili kupunguza tatizo la malaria nchini.Akitoleam fano wa Tanzania Visiwani Rais Kikwete alisema kwa upande wa Zanzibar njia hizo zimeonyesha mafanikio makubwa ambapo kwa sasa malaria ipo kwa asilimia moja.

Amesema Serikali ya Tanzania imeanzisha miradi mbalimbali ya kutokomeza ugonjwa wa Malaria ikiwa ni pamoja na mradi wa kugawa neti kwa watoto chini ya miaka mitano kwa kila nyumba ikiwa ni pamoja na kuuza neti kwa bei rahisi kwa kina mama wajawazito.Pia amesema kwa kushirikiana na Serikali ya Cuba wameanza mradi wa kunyunyuzia dawa ya kuulia mbu katika mazalia ambapo mradi huo umeonyesha mafanikio katika kanda ya Ziwa Wilaya za Muleba na Karagwe.

Rais Kikwete alisema mradi huo wa kunyunyuzia dawa katika Wilaya mbalimbali nchini unaendelea na hivi karibuni unyunyuziaji wa dawa ndani ya nyumba utaanza hivi karibuniWakati huohuo Baloziaalumu wa Malaria katika Umoja wa Mataifa ambaye pia ni mwanamuziki wa Afrika Kusini Yvonne Chakachaka amesema amekuwa akiitumia sauti yake katika kuelimisha jamii kuhusu madhara ya ugonjwa wa Malaria.

Chakachaka ambaye hivi karibu alikuwa Mtwara amesema wananchi wa mkoa wa Mtwara wamepiga hatua kubwa katika kupambana na ugonjwa wa Malaria na kuisifu Serikali ya Tanzania katika juhudi zake za kupambana na ugonjwa huo.

Pia aliiomba Serikali ya Tanzania kuendeleza juhudi hizo na kusema kuwa watoto wa Afrika wanawaangalia wao kama watu wa kuwasaidia katika kupambana na gonjwa hilo hatari.Alisema wanataka kuona Afrika inazaliwa upya na kuwa salama kutokana na ugonjwa wa Malaria kwani kwa kufanya hivyo maendeleo ya haraka yatapatikana.

No comments:

Post a Comment