header

nmb

nmb

Tuesday, May 4, 2010

CHAKACHAKA KUENDELEA KUPAMBANA NA MBU WA BONGO!!


Kiwanda cha A to Z cha mjini Arusha kimetoa msaada wa vyandarua elfu 12 kwa shule za bweni za msingi na sekondari .ili kuunga mkono kampeni ya kitaifa ya kutokomeza ugonjwa wa malaria nchini.Akitangaza msaada huo mkurugenzi mkuu wa kiwanda hicho DIVYESH RAMANANDI amesema msaada huo unalenga kuboresha afya za watoto kwa kuwakinga na kuwalinda na ugonjwa wa malaria ambao unaongoza kusababisha vifo vingi vya watoto nchini.Naye malkia wa Umoja wa Mataifa wa kupambana na ugonjwa wa malaria barani Afrika Chakachaka amelitaka bara zima la Afrika kusaidia kutokomeza malaria barani Afrika badala ya kazi hiyo kuwaachia wahisani peke yao.CHAKACHAKA amesema ugonjwa wa malaria unaweza kutoweka barani Afrika kama kila mtu yakiwemo mashirika na makampuni ya biashara yatachagia kuboresha usafi wa mazingira pamoja na upatikanaji wa dawa za kinga na tiba za ugonjwa huo.

No comments:

Post a Comment