header

nmb

nmb

Friday, April 16, 2010

Waraka wa Mtikila wamfikisha polisi, laptop yake yabebwa...........



Mwenyekiti wa Democratic Party (DP), Mchungaji Christopher Mtikila ameendelea kupata misukosuko ambapo tena ametiwa mbaroni kwa tuhuma za makosa mbalimbali ya jinai na kuwekwa chini ya ulinzi wa polisi wenye silaha.


Mchungaji Mtikila alikamtwa jana nyumbani kwake eneo la Mikocheni jijini Dar es Salaam.
Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam Bw. Suleiman Kova aliwambia waandishi wa habari jana kuwa jeshi la polisi linamshikilia kwa nia ya kumfanyia upekuzi na uchunguzi zaidi baada ya kuapata taarifa ya kujihusisha na makosa ya jinai.


"Najua kwamba mnajua Mchungaji Mtikila tumemkamata na nilijua mtaniuliza hivyo nathibitishwa kukamatwa kwake kwa tuhuma mbalimbali za jinai na mpaka sasa tunamfanyia upekuzi nyumbani kwake na sehemu za jirani lakini kiyuo cha polisi tutakachomhifadhi siwezi kukisema sasa,"alisema.


Mchungaji Mtikila ambaye ambaye anakabiliwa na kesi mbalimbali zikiwemo za kumkashifu Rais Jakaya Kikwete kwa kumuita gaidi ambapo alikamatwa na polisi na kusota rumande takribani wiki mbili kabla ya kupata dhamana.


No comments:

Post a Comment