Na Speciroza Joseph
Katibu Msaidizi wa timu ya Simba, Mohamed Mjenga jana amerudisha fomu ya kugombea nafasi ya ujumbe wa kamati ya utendaji wa timu hiyo katika uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika mwezi Mei 9 mwaka huu.
Katibu Msaidizi wa timu ya Simba, Mohamed Mjenga jana amerudisha fomu ya kugombea nafasi ya ujumbe wa kamati ya utendaji wa timu hiyo katika uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika mwezi Mei 9 mwaka huu.
Mjenga amekuwa miongoni mwa wanachama 28 wanaowania nafasi hiyo ambayo inayohitaji wajumbe tisa, wawili wa kuteuliwa mmoja viti maaluna na sita wa kuchaguliwa.
Akizungumza kuacha nafasi hiyo kubwa ya uongozi klabuni hapo, Mjenga amesema waliochukua fomu katika nafasi za juu ni watu wake wa karibu hivyo ameamua kugombea katika nafasi ya ujumbe ili kutoleta tofauti yoyote kati yake na watu wake wa karibu.
"Sijachukua nafasi za juu ili kuepusha mgongano kati yangu na marafiki zangu kwani wao wamewahi kuchukua fomu katika nafasi hizo, nimeamua kuwapa nafasi nami niende katika nafasi nyingine". alesema Mjenga.
Akizungumzia kutotomiza lengo lake katika uchaguzi uliopita wa kuhakikisha Simba inakarabati jengo lake alisema ule mpango ulikwamishwa na mmoja wa viongozi waliokuwa madarakani kwa kutokuwa mwaminifu.
"taratibu zote zilifanyika, tukapata mkataba na International Commercial Benki lakini mmoja wa viongozi wa klabu akaenda kinyume na taratibu hivyo uongozi wa benki hiyo ukasema watasaidia pindi kutakapokuwa na uongozi wa uaminifu" alisisitiza Mjenga.
Mwisho kurudisha na kuchukua fomo ilikuwa jana jioni, waliochukua fomu katika nafasi ya mwenyekiti ni Hassan Dalali anayetetea nafasi yake, wengine ni Ismail Rage, Mohamed Nanyali, Andrew Tupac, Michael Wambura, Zacharia Hanspope na Hassan Othman 'Hasanoo'.
Wanaowania nafasi ya makamu mwenyekiti ni Katibu wa sasa Mhina Kaduguda na Godfrey Nyange 'Kaburu', baadhi ya wagombea nafasi za wajumbe wa kamati ya utendaji ni Boniface Wambura, Mjenga, Selemani Zakazaka, Said Pamba, Sheikh Shughuli, Said Kubenea, Vitus Lupagiwa, Charles Hamka, Shaaban Mnyeye, Shaaban Geva, Fransis Mwenda na Ibrahim Masoud 'Maestro'.
Nafasi ya ujumbe wamejitokeza wanawake wawili Jasmin Soud na Zena Kawambwa.
Mwisho.
No comments:
Post a Comment