header

nmb

nmb

Sunday, April 11, 2010

MAMBO YA MIKASA ,WIKI HII NI WANABABA NA NYUMBA NDOGO!!


Wapendwa wasomaji wa safu hii nyeti inayozungumzia mambo mbalimbali yahusiyo jamii, mapenzi na ndoa kwa lengo la kuelimisha leo nipo tena pamoja nanyi katika kona hii nyeti.


Katika mada yetu ya wiki iliyopita nilizungumzia dalili zinazoashiria kukatika kwa uchumba na athari zake. Nina imani kila mmoja alifurahia mada hiyo.


Katika mada yetu ya leo nitazungumzia sababu zinazosababisha wanaume kutafuta nyumba ndogo na athari zake hapo baadaye.


Kwanza kabisa ni lazima tujue maana ya nyumba ndogo ni nini kwani wapo watakaodhani kuwa ni jengo dogo lilojengwa ili mwanadamu aishi humo au afanyie shughuli zake nyingine.


Lakini tunapoongelea katika suala la mapenzi "Nyumba ndogo " humaanisha kuwa ni ile hali ya mwanaume anayeishi na mkewe anapopata mpenzi mwingine nje na kumthamini kama mke mwingine hata zaidi ya mkewe anayeishi naye.


Tabia ya mwanaume kuwa na "nyumba ndogo" imekuwa ni kitu ambacho kimezoeleka japokuwa ni tabia isiyopendeza.
Kuna sababu nyingi ambazo husababisha kuwepo kwa nyumba ndogo, ambazo tunaweza kuzigawa katika mafungu tofauti, zipo zile sababu zinazosababishwa na tabia binafsi ya mwanaume kupenda sana wanawake na kutoridhika kuwa na mke wake tu .


Pili sababu zinazosababu zinazosababishwa na tabia binafsi za mke ambazo husababisha mume asiye mvumilivu kuamua kutafuta nyumba ndogo akifikiri kuwa kufanya hivyo ndivyo njia ya kutatua tatizo lililopo au kujiliwaza dhidi ya matatizo yaliyopo.


Tusiegemee tu kuwalaumu wanaume, embu tuangalie zile sababu ambazo husababishwa na mwanamke ambazo kwa kiasi kikubwa husababisha mume ndani ya nyumba kuamua kutafuta nyumba ndogo.


HASIRA NA UAMUZI WA HARAKA BILA KUFIKIRIAKuna usemi wa kiswahili usemao "Hasira ni Hasara"Katika suala la mapenzi ni vyema kuwa makini sana pale mtu unapo kasirika, iwe umemtendea au umetendewa vibaya na mwenzio.


Ni ukweli usio pingika kwamba hakuna mwanadamu asiyekasirika lakini si vyema kumkasirikia mpenzi wako mara kwa mara. Wapo akina dada ambao kukasirika huchukulia kama silaha yao ili kumkomesha mwanaume.
Hali hii husababisha wanaume wengi kutokuwa na furaha ndani ya nyumba. Hujitahidi kufanya mambo ambayo yatawaondolea adha hiyo.
Hali hii kwa kiasi fulani husababisha kubadilika kwa tabia ya wanaume hao, maana hukosa amani ya kujadili lolote na wake zao wenye hasira, hali hiyo ikiendelea kila kitu huenda hovyo. Hata mipango ya maendeleo ndani ya nyumba haipangiki


Suala la kupeana unyumba huwa gumu, na hata kama litafanyika basi huwa si katika hali ya furaha na mara nyingi ni upande mmoja tu ndio hifaidika (wanaume) tena katika hali ya kulazimisha. Hata hivyo huwa si katika hali ya furaha kamili.


Hali hiyo ikiendelea hata huyo mwanaume naye huchoka na huanza kufikiria ni jinsi gani atapata furaha kama alivyokuwa akipata mwanzo.


Katika hali hii ni rahisi sana kwa mwanaume huyo kushawishika ikiwa atajitokeza mwanamke mwingine ambaye atataka kufanya naye urafiki.


Mwanaume akipata mwanamke mwingine akashibana kimapenzi akaliwazwa na kusahahu adha yote aipatayo nyumbani kimapenzi basi penzi hilo hukomaa na kuzaliwa nyumba ndogo.


Mwanamke huyo akiwa atafanikiwa kugundua kosa lake, basi mara nyingi huwa tayari ameshachelewa na huwa panahitajika kazi ya ziada kumuachanisha mume huyo na mpenzi wake wa nje kwa kuwa wapenzi hawa wapya huwa tayari wamekwisha fanya mambo mengi ambayo huzidi kuwaunganisha pamoja .


Mambo hayo ni kama vile kuzaa pamoja, kuanzisha biashara pamoja, kumjengea nyumba na kadhalika.


MWANAMKE KUDAI TALAKA MARA KWA MARA.Kuna baadhi ya wanawake ambao kila kunapotokea mtafaruku na waume zao hudai talaka, kitendo cha kudai talaka wengine kwa makosa madogo humfanya mume kutokuwa na imani na mkeo huyo.


Jambo hilo humjengea hofu mwanaume na kumfanya afikirie kuwa na mke aliyenaye ni wa kupita tu"wakati wowote anaweza kuniacha"
Katika suala hili akina mama wenye tabia hii wanashauriwa kuacha tabia hiyo ya kutishia kutaka kuondoka . Maana kwa kufanya hivyo pasipo kujua hujikuta wakijikomoa wenyewe.
KUNYIMWA UNYUMBA.Ni jambo lisilopingika kwamba kati ya mambo muhimu kabisa yanayokamilisha furaha ya ndoa ni unyumba .Ugomvi mwingi ndani ya nyumba umekuwa ukisababishwa pia na ile hali ya wana ndoa kunyimana unyumba.


Na Wapenzi wawili walio korofishana mara tu wafanikiwapo kupeana unyumba, basi husahau tofauti zao na kuzidi kupendana zaidi.
Kuna akina mama wengine huamua kuwakomoa wanaume zao kwa kuwanyima unyumba na tena wengine kujisifia hata mbele ya mashoga zao kwamba "Siku hizi hapati kitu yeye si anajifanya mjanja nimemkomoa.".


Kwa asili ya wanaume wengi wanaumbwa katika hali ya kuhitaji unyumba zaidi kuliko ilivyo kwa wanawake. Wanaume ambao bado hawajaoa huwa ni wavumilivu kiasi fulani ukilinganisha na wale waliokwishaoa.


Kwa hiyo wanaume walioa kunyimwa unyumba na wake zao huwa ni mateso makubwa kutokana na jinsi walivyozoea kuliwazwa kwa tendo hilo. Uvumilivu ukishindikana hutafuta nyumba ndogo hata kama hakuwa na tabia hiyo.


Wapendwa wasomaji wa safu hii leo ninaishia hapa katika kipindi chetu kijacho nitawajia na mada inayozungumzia kutoridhishwa kimapenzi na athari zake
Kwa maoni na ushauri zaidi nitwangie kupitia Email gladnessmboma@yahoo.com

No comments:

Post a Comment