header

nmb

nmb

Tuesday, April 27, 2010

MWENEZI WA CCM TAMBWE HIZA ASIMIKA MAKAMANDA UVCCM ,NI MTONI KIJICHI!!

Katibu mwenezi makao makuu ya CCM Tambe Hiza (kushoto) akimvika koti mmoja waTambwe asimika makamanda UVCCM Temeke


WANACHAMA wa CCM kote nchini wametakiwa kuwa makini kupitisha wagombea wanaokubalika kwa wananchi katika nafasi za madiwani na Wabunge katika kura za maoni.
Kaimu Mkuu wa Kitengo cha Propaganda cha CCM, Bw. Richard Tambwe Hiza akisimika makamanda wa Umoja wa Vijana (UVCCM)Kata ya Mbagala na Yombo, juzi alisema wanachama wakiwapitisha wagombea wasio kubalika kutawapa mwanya wapinzani kupata nafasi za kuteuliwa kwa wingi.
Aliwataka akinamama kutokaa kimya wanapogundua njama za kuwapigia kura za maoni wagombea wasio na sifa kampeni zinazofanywa na baadhi kwa manufaa yao ambao matokeo yake ianawapa nafasi wapinzani kushinda.
"Akinamama muwe wa kwanza kuwakataa wagombea msiowakubali kwa sababu mkiwaachia wapinzani kushika viti vingi hata nafasi zao katika uteuzi wa viti maalum unaangalia asilimia waliyopata "alisema Bw. Tambwe.
Alisema CCM imejipanga kwa ajili ya uchaguzi Mkuu ambako itagawa magari kwa makatibu wa wilaya nchini na mikoa 26 nchini kwa ajili ya kukimarisha chama.
Bw. Tambwe alisema kila mwanachama wa CCM ajitokeze siku ya kupiga kura kwa sababu kura yake inakifanya chama hicho kishike madaraka kwa kura nyingi.
"Wanaccm nawadharisha kuwa ni lazima kila sehemu tumpate mgombea anayekubalika,tukifanya makosa, nafasi ya viti maalum ambayo sasa imeongezeka kutoka 68 hadi 100 tutagawana na wapinzani"alisema Tambwe.
Bw. Tambwe akiwaasa vijana katika utendaji wao aliwataka wasiwe na jazba wakati wa kampeni za uchaguzi kwa sababu chama kinawaamini kama walinzi wanaotegemewa kuwaongoza wengine.


Alisema utaratibu wa sasa wa kusimia kura zitafanywa na Kamati za uchaguzi zitachaguliwa kutoka Kata husika na mgombea atajua kura alizopata katika eneo lake.
Katika hafla hiyo makanda 11 wa UVCCM wa Kata ya Mbagala na wanne kutoka Kata ya Vutuka walisimikwa Ukamanda.

No comments:

Post a Comment