header

nmb

nmb

Saturday, April 24, 2010

KWA HILI SPIKA ALIMUWA NA HAKI YA KUTETEA WANYONGE

Waziri wa Madini
SPIKA wa Bunge Bw. Samuel Sitta jana alilazimika kutofautiana na Mwanasheria Mkuu wa Serikali akisema kuwa analinda maslahi ya Watanzania ambao watalazimika kuhamishwa katika maeneo yao baada ya kugundulika kuwa na madini.

Mvutano huo ulitokea kwenye kipengele hicho wakati kamati ya Bunge ikipitisha vifungu vya muswada huo ambapo, Spika Sitta alisema kuwa ni lazima waangalie namna ya kulinda maslahi ya Watanzania katika suala hilo na sio Mtanzania kuhamishwakwenye eneo lake akiwa masikini huku mwekezaji akitumia eneo hilo kupata mabilioni ya fedha.

Kipengele hicho awali kilieleza kuwa mwananchi huyo atalipwa gharama za usumbufu pamoja na mazao yatakayokuwepo.Katika hilo, Spika Sitta alisema kuwa: “Kweli hapa ni lazima wananchi wapewe haki haki zao kwa nini alipwe mazao peke yake? Iangaliwe thamani ya madini iliyopo ilinaye anufaike kwa kuwa ardhri hiyo itakuwa imepanda thamani,” alisema.

Kutokana na kauli hiyo, Mwanasheria Mkuu Jaji Fredrick Werema alisimama na kupinga hatua hiyo akisema inakwenda kinyume na sheria za nchi ambazo zinaeleza kuwa madini madini ni mali ya serikali.

Katika kutofautiana na hilo Spika Sitta alikataa maelezo hayo na kubaki na msimamo wake akitaka mwananchi apate fidia inayokwenda sambamba na thamani ya ardhi hiyo. “Ndugu yangu utungaji wa sheria ni siasa ni lazima tuangalie maslahi ya wananchiwetu hatuwezi kukubali wananchi waondoke wakiwa masikini huku mwekezaji akibaki na utajiri hivyo lazima kipengele hicho kilinde maslahi ya wananchi,” alisema SpikaSitta.

Baada ya kutoa msimamo huo, Jaji Werema alisema kuwa “Kweli hii kazi ni ngumu sana,” alisema na kukaa. Mambo mengine ambayo yalikubalika katika muswada huo ni pamoja na kuundwa kwa Wakalawa ukaguzi ambayo itakuwa na uwezo wa kukagua madini migodini ili kuweza kubaini mapato halisi yanayopatikana.

Suala jingine ambalo lilikataliwa ni Waziri au Serikali kufanya mazungumzo na mwekezaji katika suala la madini na kilichokubaliwa katika marekebisho ni timu ya serikali kufanya mazungumzo hayo.

Awali Waziri wa Nishati na Madini Bw. William Ngeleja alisema sekta ya madini ni moja ya sekta ambazo zimesadia nchi katika kuleta maendeleo mbalimbali yakiwemo ya barabara, afya na huduma zingine za kijamii.

Waziri alikuwa akijibu hoja za wabunge waliochangia muswada huo ambao walitaka Serikali ikubali kufanya marekebisho mbalimbali kwenye baadhi ya vifungu ili kuhakikisha sheria hiyoinatekelezeka kwa maslahi ya Watanzania.

Alisema kuwa Serikali imekuwa ikikusanya kodi na ushuru mbalimbali kutoka kwa wenye migodi ukiacha malipo ya mrahaba hali iliyochangia maendeleo hayo kwa vile taifalimejielekeza kupanua uchumi mkubwa na kwamba sio rahisi kwa mtu mmoja mmoja kuona maendeleo hayo.

Akijibu hoja za wabunge ambao walipendekeza kupunguzwa kwa mamlaka aliyopewa Waziri wa Madini pamoja na Kamishina, alisema kuwa nafasi hizo ni za kitaasisi hivyo maamuzi yatakayotolewa hayatakuwa ya mtu binafsi bali yatazingatia ushauri wawasaidizi ambao wametajwa katika sheria hiyo.

Kuhusiana na suala la kuacha mrahaba katika maeneo ambayo madini yanachimbwa alisema kuwa hatua hiyo itafanyika baadaye kwa kuwa kipindi hiki Taifa linahitaji zaidi fedha za madini kwa ajili ya kufanyia shughuli zake mbalimbali.

Kuhusiana na suala la uundwaji wa bodi ya ushauri, Bw. Ngeleja alisema kuwa serikali italiboresha suala hilo ili Waziri aweze kuwajibika kwa kutoa sababu kwenye bodi hiyo lakini pia akakubali suala la utoaji wa leseni kufanywa na makamishna wa Kanda badala ya kuja kwa Kamishna wa Madini kama ilivyokuwa imewekwa awali katika muswada huo.

Akizungumzia suala la kuwaendeleza wachimbaji wadogo alisema kuwa Serikali italifanyia kazi kwa kuwapa mahitaji muhimu kama elimu mitaji, lakini pia akawaomba wachimbaji hao kutoa ushirikiano wakati watakapotakiwa kufanya hivyo.

Mambo mengine muhimu ambayo wabunge walishauri yaingizwe kwenye sheria hiyo ni pamoja na kuwepo kwa mamlaka ya madini, mfuko wa madini ili kufanya kuwepo na usimamizi mzuri.

Pia waliomba mrahaba ubaki kwenye eneo ambalo yanachimbwa madini hayo ili kupunguza umaskini kwa watu ambao wanazunguka migodi hiyo kuliko ilivyo sasa hivi ambapo maeneo yanayochimbwa madini wananchi wake wanakuwa maskini na kukosa huduma muhimuza kijamii.
Mbunge wa Ukerewe, Getrude Mongella (CCM) katika mchango wake alitoa mfano kuwa watu wa Geita sehemu ambako kunachimbwa madini na kampuni ya Geita Gold Mine ambapo alisema kuwa wananchi wake wanaendelea kuwa maskini mbali na kuwepo kwa utajiri wa madini.
Alisema asilimia 60 wa wananchi wa eneo hilo ni maskini wa kutupwa.
Kutokana na hali hiyo aliitaka Serikali kujiandaa kurudisha madini kwa Watanzania na akaitaka Serikali kutoogopa kurudisha raslimali hiyo kwa wananchi wake kwani ni utajiri ambao wamepewa na Mungu kwa manufaa ya taifa laio.

Mbali na hayo alitaka ziwepo juhudi za makusudi za kuwasaidia wachimbaji wadogo ili hatimaye waweze kuwa wachimaji wakubwa ambao watakuwa na uwezo wa kuwekeza katika migodi mikubwa.

Naye Mbunge wa Ulanga Magharibi Dk Juma Ngasongwa (CCM) alishauri wizara ya madini kuziwezesha STAMICO na shirika la maendeleo (NDC) kwani ndio ambao watahusika kusimamia sekta ya madini ikiwa ni pamoja na kumiliki hisa ambazo Serikali itakuwanazo katika migodi mbalimbali. “Bila kutumia vyombo hivyo serikali inashikaje hizi hisa?.
Cha msingi hapa ni kuwaundia mazingira mazuri kwa kuwapa fedha na wataalam wenye uwezo bila kufanya hivyo tutaendelea kupunjwa katika hili eneo nyeti lililobeba uchumi," alisema.By.Maelezo Dodoma

No comments:

Post a Comment