header

nmb

nmb

Monday, April 12, 2010

KESI YA KUVUNA NA KUPANDA (DECI) YAKWAMA MAHAKAMANI TENA !!

WAZIRI WA HELA
HABARI KAMILI
KESI inayowakabili vinara wa Kampuni ya Development Entrepreneurship Community Initiative (DECI), imeshindwa kusikilizwa kutokana na jalada la kesi hiyo kushindwa kupangiwa hakimu.
Jalada la kesi hiyo lilikuwa Mahakama Kuu kwa ajili ya kushughulikiwa dhamana ambapo hivi sasa limerejeshwa Mahakama ya Kisutu na bado halijapangiwa hakimu.
Awali washitakiwa katika kesi hiyo waliandika barua ya kumkataa Hakimu Mkazi wa Kisutu, Aloyce Katemana, kwa madai kuwa hawana imani naye.
Akiahirisha kesi hiyo Hakimu Katemana amesema Mahakama imeshindwa kusikiliza kesi hiyo kwa kuwa hakimu wa kusikiliza bado hajapangiwa.
Hakimu amesema ameamua kujitoa ili haki itendeke baada ya washitakiwa kumuomba afanye hivyo.
Washitakiwa hao ni Jackson Mtares, Timotheo Ole Loitg'nye, Swamel Mtares na Arbogast Kipilimba wakazi wa Dar es Dar es Salaam.
Kwa pamoja vinara hao wanashitakiwa kwa wizi wa sh. milioni 118 kutoka kwenye akaunti ya kampuni hiyo. Kesi hiyo itatajwa tena Mei 10, mwaka huu.

MIPESA YA KUVUNA

No comments:

Post a Comment