MELI YENYEWE
HABARI KAMILI
HOFU ilitawala katika meli ya Flying Horse iliyokuwa ikitoka Zanzibar kuja Dar es Salaam baada ya kuvumishwa kuwa imepata hitilafu na kwamba inazama, hali iliyosababisha abiria kadhaa kuzirai.
Kwa mujibu wa abiria mmoja aliyekuwamo ndani ya meli hiyo ambaye hakutaka jina lake liandikwe gazetini amesema tukio hilo limetokea saa nne usiku wa kuamkia leo wakati meli hiyo ikiwa imepakia abiria na ikijiandaa kung’oa nanga.
Abiria huyo amesema uvumi huo ulizushwa na kijana mmoja aliyekuwa abiria ambaye anadaiwa kuwa na matatizo ya akili.
Imedaiwa kuwa mara baada ya abiria huyo kuanza kutangaza kuwa meli hiyo imepata hitilafu, abiria wenzake walianza kukumbwa na kiwewe huku wengine wakijikusanya pamoja na kuanza kufanya maombi kwa ajili ya kuepushwa na ajali hiyo.
Heka heka hizo zilisababisha abiria kadhaa kuzirai lakini baadaye walipata huduma ya kwanza na kurejea katika hali yao ya kawaida.
Wakati wengine wakiendelea kufanya hivyo baadhi ya abiria walikuwa wakitafuta mbinu mbalimbali za kujiokoa kwa kutumia vifaa maalumu vya kuogelea.
Wakati hekaheka hizo zikiendelea, baadhi ya ndugu na jamaa walikuwa wakipiga simu ili kujua hatima ya ndugu zao huku wengine wakiwasiliana na uongozi wa meli hiyo.
Wakati hayo yakiendelea, uongozi wa meli hiyo uliwatangazia abiria kuwa meli hiyo haina tatizo na kwa yeyote mwenye hofu zaidi anaweza kurudishiwa nauli ili ajipange upya.
“Tunaomba ndugu zetu abiria uvumilivu uwepo,” lilisikika tangazo likisema na kuongeza, “Huo ni uvumi tu. Kwa yeyote mwenye mashaka na safari hii aseme mapema arejeshewe nauli ili wengine waendelee na safari zao.”
Maofisa wa meli hiyo walieleza kuwa ni vigumu kwa meli hiyo kuzama kutokana na uvumi kuwa ilikuwa imejaza sana kwani vipimo vilionesha kuwa haikuwa na uzito mkubwa kiasi cha kuizamisha.
Hata hivyo, imedaiwa kuwa uvumi huo ulienezwa na abiria mmoja ambaye anadaiwa kuwa na ugonjwa wa akili ambaye ametiwa mbaroni na polisi kutokana na mkasa huo.
Meli hiyo hufanya safari zake kila siku na iliweza kuendelea na safari na kufika salama jijini Dar es Salaam.
nanga.

RAMANI YA NJIA YA MELI
No comments:
Post a Comment