MSANII Profesa. J akiwa na wadau mwa globu hii Spear Patrick kushoto na Mzee Peter Mwenda kulia habari maelezo leo ktk kuzungumzia tamasha la tarehe 13 mwezi February linaloitwa "zinduka" litakalofanyika katika viwanja vya Leaders’ Club jijini Dar es salaam.
Joseph Haule amesema Tushirikiane Kuitokomeza, kauli inayowataka watanzania kujikinga wao na familia zao dhidi ya malaria.Baadhi ya wasanii walio saini katika uzinduzi huu wa Malaria Haikubaliki ni pamoja na; Kidumu, Diamond, Dully Sykes Marlaw, Professor Jay, Lady Jay Dee, Mwasiti, Bi Kidude, Banana Zoro, Ray C, Maunda Zoro, Tanzania House of Talent (THT) dance troupe, Banana, amini na pipi, Mataluma na R Tony.Tiketi za kuingia kwenye tamasha la zinduka zinauzwa kwa shilingi (3000) na zitapatikana zuzu, Steers -Millenium Tower na Town Outlet.
Msanii Prof. J akizungumzia tamasha la tarehe 13 mwezi February linaloitwa "zinduka" litakalofanyika katika viwanja vya Leaders’ Club jijini Dar es salaam huku mgeni rasmi atakuwa mheshimiwa Raisi Jakaya Mrisho kikwete akiongoza kampeni ya Malaria Haikubaliki
Zinduka itasaidia kutokomeza Malaria Haikubaliki 2010 na pia itawezesha shughuli zote za mwaka huu, tamasha litarushwa hewani moja kwa moja na vituo vya luninga na redio vinavyowafikia mamilioni ya watanzania na ujumbe mahususi ni kila mmoja kujua jukumu lake katika kuzuia malaria.Kwa kuongezea wasanii mahiri 18 wametengeneza wimbo maalumu unaohusu malaria na unachezwa katika vituo mbalimbali vya redio, huu ni ushirikiano mkubwa wa wasanii ambao haujawahi kuwapo hapa Tanzania, na siku ya Tamasha wimbo huo utaimbwa laivu
Muziki una nguvu kubwa katika kuelezea historia ya Tanzania katika kupambana na malaria na kuonyesha mafanikio yetu katika kupambana na gonjwa hili”alisema msemaji wa kampeni hii Lady Jay Dee. “katika tamasha la zinduka,watanzania woe watapaza sauti zao kwa wimbo kutoa wito wa kutokomeza janga la malaria nchini.Tanzania itakuwa nchi ya kwanza katika nchi za Afrika kufanikisha utumiaji wa vyandarua vya mbu na tiba ya gharama na nafuu kwa raia wake.Katika kutoa ushirikiano wa zoezi hili Malaria Haikubaliki inahamasisha sekta zote za kijamii pamoja na ulimwengu wa burudani, biashara, michezo na dini kuungana pamoja katika kutokomeza malaria na kusaidia kupunguza vifo vinavyosababishwa na malaria nchini kote.Kwa mwaka wote wa 2010, kampeni itafanya kazi kuongeza vitendo vya nadharia katika kuzuia malaria kama vile kulala muda wote ndani ya chandarua kilichowekwa dawa,kuitambua na kuitibu malaria mapema na kuwajali wamama wajawazito.
Malaria Haikubaliki itafanikisha hili kwa kutoa elimu juu ya malaria na ufahamu, pia kuhamasisha shughuli za pamoja katika jamii, PSAs, ujumbe mbalimbali kwa njia ya redio na luninga,mabango,levo za utamaduni katika jamii na matamasha ya michezo na pia maonesho ya barabarani,lengo kuu likiwa ni kuhakikisha kila familia nchini imesikia ujumbe kwamba malaria haikubaliki.Inakadiriwa kila mwaka watu eflu sitini hufa kwa malaria nchini Tanzania na waathirika wakubwa ni watoto walio chini ya umri wa miaka mitano.
Malaria Haikubaliki: Tushirikiane Kuitokomeza inaongozwa na serikali ya Tanzania na wizara ya afya na ustawi wa jamii.washiriki wengine wa kampeni hii ya malaria ni Roll Back Malaria Partnership, Malaria No More, Population Services International, Johns Hopkins University Center for Communication Programs, Tanzanian Red Cross, United Against Malaria, MEDA Christian Social Services Commission, Bakwata (the National Muslim Council) na World Vision, wakishirikiana na the Global Fund to the Fight AIDS, Tuberculosis na Malaria na the U.S. President’s Malaria Initiative.
No comments:
Post a Comment